BANDA MEDIA BLOG

SERIKALI YAKEMEA VITENDO VYA KUWAFUKUZA KAZI NA KUWATANGAZA KWENYE VYOMBO VYA HABARI WATUMISHI WA UMMA- TALGWU YAIPA 5

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete,akizungumza  wakati akifungua kikao cha 30 cha Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kilichofanyika leo Januari 15,2025 jijini Dodoma.

                                                                       .........................

NA JOHN BANDA, DODOMA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Ridhiwan Kikwete, amekemea kitendo cha baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiwafukuza kazi na kama haitoshi wanawadhalilisha kwa kuwatangaza kwenye vyombo vya Habari Watumishi wa Umma

Kikwete ametoa kalipipio hilo wakati akifungua mkutano wa 30 wa Baraza la wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) jijini Dodoma, Januari 15,2025 ambapo amesema vitendo hivyo ni vya udhalilishaji na havikubaliki.

“naomba kutoa maagizo kwa wale ambao wameendelea kunyanyasa na kuwadhalilisha baadhi ya watumishi wa serikali, kwa kuwatangaza kwenye majukwaa na kama haitoshi wanawatangaza na kwenye magazeti vitendo hivi vya udhalilishaji havikubaliki waache mara moja”, amesema

Aidha amesema waajili wote wanaofanya hivyo waache mara moja, ambapo kinachokera na kudhalilisha zaidi ni kitendo cha kutangaza mpaka sababu zilizosababisha kufukuzwa kwak 

 Kwa Upande wake Katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), Rashid Kitima akisoma risala ya chama hicho ameipongeza serikali kwa  Kusikia kilio cha muda mrefu cha Chama kwa Watumishi waliokuwa wanalipwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri na sasa wameanza kulipwa moja kwa moja kupitia mfuko mkuu wa Serikali, Pamoja  na pongezi hizo chama kinaendelea kuiomba Serikali kuwahamishia Hazina watumishi waliobaki wakilipwa kwa mapato ya ndani 

Ametoa pongezi nyingine kuwa ni Pamoja na serikali Kuendelea kuwapandisha madaraja Watumishi wa Umma na kuajiri kwa wingi Watumishi wa kada mbalimbali hususan Watumishi wa kada ya Afya, ikiwa ni Pamoja na kushughulikia madai mbalimbali ya watumishi yatokanayo na mishahara (arrears), kwani chama kimeshuhudia Watumishi wengi wamelipwa malimbikizo waliyokuwa wanaidai.

 Aidha amesema serikali imeboresha kikokotoo kwa kuongeza malipo ya mkupuo kutoka 33% - 40% kwa Watumishi wa Umma na kwa kundi lingine lililopandishwa kwenda 33% na sasa kuwa 35%.  

“Tamko la Serikali lililopelekea Viongozi wa kisiasa kuacha kutumia vyombo vya habari na majukwaa katika mikutano ya hadhara kutoa matamko ya kuwadhalilisha Watumishi wa Umma kwa kuwafukuza, kuwasimamisha kazi na kuwaweka ndani”, amesema

Mwenyekiti wa TALGWU Taifa ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA), Tumaini Nyamhokya,akizungumza  wakati wa kikao cha 30 cha Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kilichofanyika leo Januari 15,2025 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa TALGWU, Rashid Mtima,akizungumza  wakati wa kikao cha 30 cha Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kilichofanyika leo Januari 15,2025 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Waziri  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati akifungua kikao cha 30 cha Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kilichofanyika leo Januari 15,2025 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  kikao cha 30 cha Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kilichofanyika leo Januari 15,2025 jijini Dodoma.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG