Video kadhaa zilichukuliwa na wapiganaji vijana wa FSR na kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii: TikTok, Twitter, Facebook... Wapiganaji hao vijana, wakiwa na silaha mikononi, wanaonekana wakivaa sare za kijeshi, huku wakijirekodi. Wanatumia kamera ya simu zao kama shahidi, wanajivunia ushujaa wao, vijiji walivyoharibu, watu walioua na kutaja tarehe, majina ya miji, vitongoji, na wale waliohusika wakitekeleza mauaji hayo.
“Ni haki yetu”
Katika moja ya video hizi, mpiganaji hurekodi barabara iliyo tupu, maiti zikiwa zimetapakaa ardhini. "Tuko katika wilaya ya al-Thawra, huko El-Geneina," anasema mmoja wa wapiganaji hao vijana, kabla ya kuongeza: "Massalits wamefanikiwa kuangamizwa, asante Mungu. »Katika video vyingine, kamanda anahalalisha ubakaji uliofanywa na askari wake: "Tukiwabaka dada zenu na binti zenu, ni haki yetu," anasema, akitazama kamera. Timu hii ya waandishi wa Gazeti la New Yprk Times pia iliweza kupata utambulisho wa mtu huyu.
Ushahidi muhimu
Kwa kuangalia shuhuda mbalimbali, waandishi wa habari na watafiti waliweza kutambua karibu makamanda ishirini wa RSF na majukumu ya kila mmoja. Ushahidi muhimu wa kuona katika tukio la uchunguzi wa kimataifa.
