BANDA MEDIA BLOG

WAZIRI MKUU AWASILI MSUMBIJI KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA UAPISHO WA RAIS CHAPO

 WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa  Januari 14, 2025 amewasili Maputo nchini Msumbuji ambapo atamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho wa Rais mteule wa Nchi hiyo Daniel Chapo utakaofanyika leo Januari 15, 2025. 

Mheshimiwa Chapo alishinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa asilimia 70.67 kupitia chama tawala cha FRELIMO dhidi ya mpinzani wake Venancio Mondlane aliyepata asilimia 20.32 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 9, 2024. 

Chapo anakuwa Rais wa tano wa Msumbiji, akichukua nafasi ya Filipe Nyusi baada ya kukamilisha mihula miwili ya utawala wake.

Sherehe za uapisho zitafanyika katika uwanja wa Independence (Uhuru) jijini Maputo.   

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG