Siku ya Redio Duniani ni siku ya kimataifa inayoadhimishwa tarehe 13 Februari kila mwaka. Siku hiyo iliteuliwa na UNESCO tarehe 3 Novemba, 2011, wakati wa mkutano wake wa 36.
Hata hivyo kwa kuthibitisha kuwa, kila tarehe 13 Februari itakuwa inaadhimishwa kutokana na kwamba, tarehe hiyo mwaka 1946 ndipo ilianzishwa Radio ya Umoja wa Mataifa. Ni katika kutumia chombo hiki cha mawasiliano na msingi wa kutoa habari ambayo inasaidia kukuza uhuru wa kujieleza na usawa wa kila kitu. Radio iweze kutoa mchango katika mijadala ya kidemokrasia kwa njia ya kubadilishana mawazo kati ya watangazaji na wasikilizaji.
Kwa sasa Redio inapitia katika upinzania mkubwa kutokana na mitandao ya kijamii ambayo imepunguza wasikilizaji...
Kwa Tanzania siku hiyo kitaifa inaadhimishwa kitaifa jijini Dodoma ambapo kutakuwa na mijadara mbalimbali kutoka kwa wataalamu mbalimbali.
Tags
MCHANGANYIKO
