Na Mwandishi wetu, DODOMA
OFISI ya Taifa ya Mashtaka, imezindua muongozo wa upelelezi na uendeshaji wa mashtaka ya makosa ya kimtandao, utakao wezesha wapelelezi na waendesha mashtaka, kushughulikia kesi za kimtandao na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa viwango vinavyofanana.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Maryprica Maundi, akizindua muongozo huo jana jijini hapa, alisema matumizi sahihi ya muongozo huo yatasaidia kudhibiti tatizo la ushughulikiaji usio sawa wa mashauri ya mtandao.
“Hususani katika vipengele vya upelelezi, unadaji wa hati za mashtaka,uendeshaji wa mashauri mahakamni pamoja na uanadaaji wa hati nyingine zinazowasilishwa mahakamani.
“Hivyo naomba nitoe rai kwa wapelelezi na waendesha mashtaka kote nchini kutumia ipasavyo mwongozo huu unaozinduliwa ili kupata mafanukio chanya katika mashauri tunayoshughulikia,”alisema Maundi
Aidha, alisema makosa ya kimtandao nchini kama ilivyo katika nchi nyingine yamendelea kwa kiasai kikubwa kila kukicha na kubadilika mara kwa mara kutokana na maendeleo ya tekonolojia.
Alisema, hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
“Pamoja na mambo mengine makosa ya mtandao huathiri ukuaji ukuaji wa uchumi na kuhatariha utawala bora na haki za binadamu miongoni mwa maeneo ambayo yanatajwa kuwa na kiwango kikubwa cha viashiria vya makosa ya kimtandao nchini ni pamoja na eneo la vyombo vya habari hususani mitandao ya kijamii, mifumo ya kopyuta kwenye mabenki na taasisi za fedha pamoja na matumizi mabaya ya mifumo yote inayotumia mtandao kwenye shughuli za kiserikali na binafasi,”alisema
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Slvester Mwakitalu, alisema muongozo huo utakwenda kuongeza tija kwenye ushughulikiaji wa makosa ya kimtandao.
Alisema kutokana na ukuaji wa sayansi na teknolojia makosa ya kimtanadao yameongezeka kwa kasi sana hivyo muongozo huo utakwenda kusadia wapelelezi na waendesha mashtaka kupata namna bora ya kushughulikia kesi za makosa ya kimtandao.
“Muongozo huu unakuja kuongeza tija katika kushughulikia makosa ya kimtandao kwani utawezesha wapelelezi na waendesha mashtaka kufanya kasi kwa viwango sawa tofauti na ilivyo sasa ambavyo kila mkoa wamekua wakifanya kwa namna yao,”alisema
Awali, Mkurugenzi Divisioni ya Utaifishaji na Urejeshaji Mali kwa Makosa yanayovuka Mipaka na Uharifu mahsusi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Faraja Nchimbi, alisema pia lengo la muongozo huo ni kuweka viwango linganifu kwa wapelelezi na waendesha mashataka.
Hata hivyo, alisema lengo jingine ni kuondoa dosari za kiutendaji wakati wa upelelezi na uendeshaji wa makosa hayo na kuboresha ushahidi unaokusanywa na kuhakikisha mafanikio ya kesi hizo zifikapo mahakamani.
MWISHO





