Mwanasheria mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johary amewataka wafanyakazi katika ofisi ya mwananasheria mkuu wa Serikali kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na Ubora kuanzia mavazi, kauli mpaka katika uwajibikaji.
Mhe. Johary ametoa maelekezo hayo wakati alipokuwa
akifungua mafunzo Elekezi ya siku mbili kwa wafanyakazi wapya wa Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali yanaofanyika jijini Dododoma kuanzia leo machi
13,2025
“tunawafundisha wafanyakazi wapya ili waweze kujua
majukukumu na wajibu ndani ya ofisi hii inayosaidia serikali,
Pia wafahamu dira, dhima pamoja na kauli mbiu yetu ya
viwango na ubora katika utendaji kazi wetu”, amesema
Jumla ya wafanyakazi 98 wa ofisi hiyo wameshiriki
mafunzo hayo ambayo yameambatana na ujazaji fomu ya kiapo Pamoja na kupata
kiapo cha utii…