BANDA MEDIA BLOG

NIT YAWEKA WAZI MAFANIKIO YAKE MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

 


Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Prosper Mgaya, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa chuo hicho katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Machi 20, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.

   

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Prosper Mgaya, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa chuo hicho katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Machi 20, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA
KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita,Chuo  Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) kimekamilisha maandalizi ya utoaji wa  kozi ya mafunzo ya Urubani ambapo kiasi Cha shilingi bilioni 6 zimetolewa na Serikali  katika maandalizi hayo.
Hayo yamesemwa leo Machi 20,2025 jijini Dodoma na Mkuu  wa chuo hicho Dkt.Prosper Mgaya,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa chuo hicho katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Dkt.Mgaya amesema Serikali ya awamu ya sita imekiwezesha NIT kukamilisha maandalizi ya mafunzo ya urubani ili kupata ithibati ya utoaji wa mafunzo ya urubani kimataifa.
 Aidha amesema kuwa ili kupata  ithibati na kuruhusiwa kutoa hayo mafunzo, lazima chuo kupitia hatua tano ambapo kila hatua inahitaji rasilimali mbalimbali inayotakiwa kuwepo.
“NIT tunaishukuru Serikali yetu kupitia uongozi thabiti  wa Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo, kati ya hatua tano tumeshakamilisha hatua nne na hatua ya tano ni ‘satification’ kwamba kuja kupewa ithibati kimataifa “
“Hatua zote tano Serikali imewekeza jumla ya shilingi bilioni 6 ili kuweza kupita katika zile hatua kwa ajili ya maandalizi ya kupita zile hatua ili tuweze kupata ithibati.”amesema 
Amesema  kama nchi imekuwa ikipeleka wataalam nje ya nchi kwenda kupata mafunzo ya urubani  ambapo Serikali na watanzania kwa ujumla wamekuwa wakitumia  fedha nyingi za kigeni kusomesha marubani nje ya nchi .
“Lakini kwa kuanzisha mafunzo hayo kwenye chuo cha Taifa cha umma cha Usafirishaji kutapunguza gharana za mafunzo hayo kwa takribani asilimia 50 hadi 60   ambazo watanzania wengi wanatumia kupata mafunzo hayo nje ya nchi.”Dkt.Mgaya
Hata hivyo amesema kuwa  kuanza kwa mafunzo hayo pia kutaokoa fedha za kigeni ambazo zimekuwa zikitumika nje ya nchi na baada ya mafunzo hayo kuanza fedha hizo zitabaki hapa nchini.
Amesema , kuanza kwa mafunzo hayo kutaongeza marubani  wazawa ambapo kutapunguza kwa kiasi kikubwa kutegemea wa majumbani wa kigeni ambao gharama yake ni kubwa

Dkt.Mgaya, amesema Serikali imenunua ndege mbili za mafunzo aina ya Cesna 172 zenye injini moja ambazo tayari zipo nchini kwaajili ya kuanza mafunzo hayo.

“Ndege hizi zina thamani bil 2.9 na serikali ipo katika taratibu za ununuzi wa ndege nyingine tatu ikiwa ndege moja ya injini mbili ambayo itawasili mwezi Oktoba 2025 ambayo ina thamani ya bil.5.9, na Ndege mbili za injini moja zitawasili mwaka 2026.”amesema 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG