BANDA MEDIA BLOG

BARABARA ZA LAMI MBINGA HADI MBAMBA BAY "NAKONDWA KUPHUNDA"

 

                            "kwa barabara hizi nakondwa kuphunda"
            

               NA JOHN BANDA, RUVUMA

WAKAZI wa Wilaya za Mbinga na Nyasa mkoani Ruvuma wamesema pamoja na Barabara zenye kiwango cha Lami zenye urefu wa kilometa 66. kuwafungulia uchumi lakini pia zimegeuka kuwa kivutio cha kiutalii kwa wageni wa mkoa huo.

Barabara hiyo iliyoanza kujengwa kwa kiwango cha lami nzito wakati wa uongozi wa Rais Hayati Dkt, John Pombe Magufuli na kakamilishwa na Rais wa Awamu ya 6 Dkt, Samia Suluhu Hassan ikizinduliwa nae septemba 25, 2024

Akiongea na Channel ya Banda Media katika Stendi ya Mabasi ya Mbamba bay Katibu Mwenezi wa CCM, wilaya ya Nyasa Stanford Nyambo (KATAPILA) amesema, Barabara hiyo imewarahisishia sana wakazi wa wilaya hiyo usafiri, kwani awali walikuwa wanataabika sana kwa kutembea umbali mrefu kutokana na kutokuwa na usafiri wa muaminika.

“ndugu mwandishi usione hivyo wananchi tulikuwa tukitembea hapa mpaka mbinga kwa miguu kwa zaidi ya siku 4, njiani maana usafiri uliokuwepo ulikuwa wa garama sana, kutokana na ubovu wa barabara hata haya makosta hayakuwa na uwezo wa kupita,

                                      "kwa barabara hizi nakondwa kuphunda"

Lakini baada ya serikali kutujengea barabara hizi imekuwa rahisi sana kusafiri na kusafirisha mazao yetu, lakini kama haitoshi ni barabara za mfano kwani kila mgeni anayezikanyaga anashangaa kwamba zipo Tanzania hi hi, zimekuwa kivitio kikubwa cha utalii”, amesema

Naye Jofrey Mlope amesema “kwa kweli mimi nilihamia hapa mbinga mwaka 2016 magari aiana ya Landrova 110 ndiyo yalikuwa yakisafirisha abaria ambapo kwa umbali wa kilometa 70 za hapa na mbamba bay zilikuwa zikitumia hadi masaa 6 kutokana na ubuvu wa barabara.

Amesema barabara hizo zilizojengwa kiustadi zinavutia kutokana na kona nyingi na za hapa pale kwani Jografia ya Mbinga na mbamba bay ni ya mito, mabonde na miinuko ndiyo maana walizikona sana wajenzi.

kwa upande wake Ernest Nindi mkazi wa kijiji cha Liuli kilichopo mwambao wa ziwa Nyasa amesema kwa kifupi kuwa kwa Barabara hizi "nakondwa kuphunda", akimaanisha anafurahishwa sana na barabara hizo akitamka kwa kabila la Wanyasa

Barabara hizo zinatajwa kujengwa na   kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd na kusimamiwa na Wakala ya Barabara – TANROADS, ukiwa na thamani ya Shilingi bilioni 122.76 huku Shilingi milioni 637.4 zikitumika kulipa fidia kwa wananchi.

Barabara ya Mbinga - Mbamba Bay inatajwa kuwa sehemu ya barabara kuu ya ushoroba wa Mtwara (Mtwara Corridor) yenye jumla ya urefu wa kilometa 826 inayoanzia Mtwara mpaka Mbamba Bay ambapo pia barabara hiyo inaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Mtwara pamoja na Mkoa wa Mbeya na nchi Jirani ya Malawi kupitia Ziwa Nyasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG