BANDA MEDIA BLOG

CCM YAZINDUA BARAZA LA WAZEE WA CHAMA HICHO


             ....................

Na Barnabas kisengi Dodoma 

April 14.  2025.

Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Jijini Dodoma kimezindua Baraza la Wazee wa chama cha Mapinduzi kata ya kilimani 

Akizundua Baraza hilo mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Dodoma Comredi Charles Mamba amesema kuwepo kwa Baraza hilo la Wazee kata ya kilimani kutaleta tija katika chama cha Mapinduzi kata na kwa viongozi na wanachama.

"Hili Baraza mmelizindua wakati mwafaka maana kilimani tunayoijua sisi hapa katikati ilianza kuharibika kwa kupoteza Maadili kwa viongozi na wanachama Sasa hili Baraza la Wazee hakikisheni mnairudisha kilimani ilipo kuwa kwakuwa Kilimani ndio imebrba sura ya kuwa Viongozi wengi wa Serikali na Chama kuishi hapa"amesema Comredi mamba

Comredi Mamba amesema kuwa Baraza la Wazee hili litakuwa likihakikisha swala la Maadili kwa wanachama na viongozi linakuwa kipaombele katika kata ya kilimani.

Awali akisoma risala ya Wazee mwenyekiti wa baraza la Wazee kata ya kilimani Mzee chambasi amesema Changamoto kubwa kwa Wazee wa kata ya kilimani ni swala la afya Wazee wengi kutokuwa na bima ya Afya, pia baadhi ya mitaa kutokuwa na miundombinu ya barabara hasa mtaa wa chinyoyo na image hali ya miundombinu sio nzuri kabisa hasa katika kipindi cha masika hali inayopelekea mitaa hiyo kujitenga kwa mawasiliano ya barabara.

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la dodoma ambaye pia ni Waziri wa Madini Mhe Anthony Peter Mavunde amekipongeza Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani kwa kuunda Baraza hilo la Wazee kwakuwa liko kwa mujibu wa katiba ya chama cha Mapinduzi 

Mhe Mavunde amewataka Wazee hao kujiorozesha vizuri wote ili aweze kujua idadi ya Wazee ambao hawana kadi za bima ili aweze kuwaunganisha kwa pamoja awakatie bima za afya

Aidha Mhe Mavunde amegusia swala la miundombinu ya barabara ya Mtaa wa chinyoyo ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa kipindi kirefu bila kupata tiba ila safari hii kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026 barabara za mtaa wa chinyoyo zitapata tiba.

"Nimekuwa nikiumia sana Kwa barabara za mtaa wa chinyoyo zinavyo watesa wananchi ila katika bajeti yetu ya mwaka huu hizi barabara tumezitengea fedha ili zitengenezwe katika ubora mzuri kupitia tarula"amesema Mavunde

Aidha Mhe Mavunde amesema kata ya kilimani tangu nchi ipate uhuru haikuwahi kuwa na Shule ya msingi wala secondary ila kwa Sasa tayari nilichangua Ujenzi wa Shule ya msingi na Sasa tuko hatua za mwisho kukamilisha Ujenzi wa Shule ya msingi na hivi karibuni tutaanza ujenzi wa Shule ya secondary.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG