Raia wasiopungua 33 wameuawa na wengine kadhaa
kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya makombora ya wapiganaji wa RSF katika
mji wa El-Fasher, makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini huko magharibi mwa
Sudan, jeshi lilisema siku ya Jumatatu.
Taarifa ya jeshi ilisema kuwa wapiganaji wa RSF
wamekuwa wakishambulia kwa makombora tangu siku ya Jumapili asubuhi.
Wapiganaji wa RSF hawajuzungumzia chochote kuhusu
tukio hilo
Mapema wiki hii, kundi hilo la wapiganaji lilidai
kuchukua udhibiti wa kambi ya wakimbizi ya Zamzam huko El-Fasher baada ya
kukabiliana na vikosi vya jeshi.
Raia wasiopungua 400 waliuawa na karibu wengine
400,000 kuondolewa katika makazi yao kutokana na mapigano, kulingana na takwimu
za Umoja wa Mataifa.
Kumekuwepo na mapigano makali kati ya jeshi la Sudan
na wapiganaji wa RSF katika eneo la El-Fasher tangu Mei 2024, licha ya jumuiya
ya kimataifa kuonya kuhusu hatari ya kupigana katika mji huo, ambao ni kitovu
cha shughuli za misaada kwa ajili ya majimbo yote matano ya Darfur.
Tangu Aprili 15, 2023, RSF imekuwa ikikabiliana na
wanajeshi wa Sudan kwa lengo la kudhibiti nchi, jambo lililosababisha mauaji ya
maelfu ya watu na kuwepo na moja ya hali mbaya kwa watu duniani.
Zaidi ya watu 20,000 wameuawa kufikia sasa, na
wengine milioni 15 kuondolewa katika makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa
na seriikali za mitaa. Hata hivyo utafiti kutoka kwa wanazuoni wa Marekani,
unakadiria kuwa waliouawa ni karibu 130,000.
CHANZO:AA
