BANDA MEDIA BLOG

RPC KATABAZI AZINDUA SUPER CUP NA KUWAFIKIA WANACHUO KUPINGA UHALIFU.

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limezindua Mashindano ya Boaz Super Cup yenye lengo la kufikisha elimu ya ulinzi shirikishi kwa makundi mbalimbali ya Jamii kupitia mchezo wa mpira ili kuiweka jamii na Jeshi la Polisi pamoja kwa lengo kupambana na uhalifu.

 Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (SACP) George Katabazi ambapo amesisitiza umoja na mshikamano kati ya jamii na Jeshi hilo katika mapambano dhidi ya uhalifu.

Aidha, Katabazi amesema Jeshi la Polisi kupitia dhana ya Polisi Jamii ina lengo la Kuifikia Jamii katika makundi mbalimbali na kutoa elimu ya kuzuia na kutanzua uhalifu kupitia michezo midahalo pamoja mikutano ya kusikiloza kero za wananchi.

Waandaaji wa Mashindano hayo Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini na baadhi ya washiriki wamesema kuna umuhimu mkubwa kwa jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kunusuru vijana wengi na wimbi la uhalifu

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG