BANDA MEDIA BLOG

BALOZI KUSILUKA AZITAKA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI KUSHIRIKIANA NA WAKAGUZI WA NDANI

 

Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka akifafanua jambo wakati alipokua akufungua Mkutano wa Mwezi wa Ukaguzi wa Ndani uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma

                             ...........................................

                          NA JOHN BANDA, DODOMA

KATIBU Mkuu kiongozi Balozi Dkt. MOSES KUSILIKA ametoa wito kwa taasisi za Umma na Binafsi  kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na kuwaamini wakaguzi wa ndani ili kusadia kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu kwa lengo la kusaidia kuondoa makosa yanayosababisha hati chafu na badala yake kuleta maendeleo chanya  katika taasisi na Taifa kwa Ujumla.

Balazi Dkt.KUSILUKA ameyasema hayo Jijini DODOMA kwenye kikao cha mwezi cha maaafisa ukaguzi wa ndani ambapo amesema ni muhimu kufanya kazi kwa kuzingatia welezdi na kufanya kazi kwa uwazi ili kufanikisha malengo ya taasisi na Taifa.

Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA) DKT. ZELIA NJEZA ameziomba  taasisi za Umma na Binafsi Nchini  kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wa ndani ili wasaidie kuwapa Elimu juu uendeshaji wa  taasisi hizo ili zifanye kazi kwenye mlengo sahihi 

 Kaulimbiu inayosindikiza kikao hicho cha wakaguzi wa ndani ni "Kuviwezesha Vyama. Kuimarisha Uaminifu. Kunyanyua Viwango vya Utendaji."

RAIS wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania, Dk. Zelia Njeza (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka baada ya kufungua Mkutano wa Mwezi wa Ukaguzi wa Ndani uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma



RAIS wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania, Dk. Zelia Njeza (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka baada ya kufungua Mkutano wa Mwezi wa Ukaguzi wa Ndani uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma jana. Kulia ni Mkaguzi Mkuu wa ndani, Benjamin Magai.



Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG