BANDA MEDIA BLOG

PAPA LEO XIV ATANGAZA KUWA KANISA KATOLIKI HALITABARIKI TENA NDOA ZA JINSIA MOJA


 Papa Leo wa XIV ametangaza kwamba Ndoa ni Muungano kati ya mwanaume na mwanamke. Hiyo ndiyo ndoa pekee inayokubalika mbele za Mungu. Kanisa Katoliki halitabariki tena ndoa za mashoga.

Papa Leo pia amesema kuwa kutoa mimba ni kitendo cha kishetani na kiovuYeye anapinga kabisa jambo hilo.

Katika hotuba yake ya kwanza kwa mabalozi wa Vatican Jana Mei 16, 2025, Papa Leo XIV alisisitiza mafundisho ya jadi ya Kanisa Katoliki kuhusu ndoa na uhai. Alisema kuwa familia inapaswa kuanzishwa juu ya "muungano thabiti kati ya mwanaume na mwanamke" na akathibitisha hadhi ya asili ya watoto ambao bado hawajazaliwa pamoja na wazee .

Pia, Papa Leo alisisitiza msimamo wa Kanisa dhidi ya utoaji mimba na Euthanasia, akivitaja kama sehemu ya "utamaduni wa kutupa" wa kisasa. Hata hivyo, alisisitiza kuwa watu wa LGBTQ+ wanakaribishwa katika Kanisa, ingawa mafundisho rasmi kuhusu ndoa na vitendo vya ushoga havijabadilika .

Mudumoh ✍️

#halisinewsflash

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG