BANDA MEDIA BLOG

PAPA WA SASA AMECHAGUA JINA LA LEO, LEO NI NANI HASA???


Mtakatifu Leo ni nani? Ni Leone Magno mzaliwa wa Tuscany Roma Italia mnamo mwaka c 400 na kufariki 10 November 461.

Huyu ndiye papa wa kwanza kujulikana kwa jina la The Great “Papa Mkuu”, wengine waliowahi kuitwa the Great Popes Gregory I na Nicholas I.

Mwaka 1754 Pope Benedict XIV alimtangaza Pope Leo 1 kama Daktari wa Kanisa kutokana na mchango mkubwa wa mabadiliko ya kitheolojia ndani ya kanisa. Moja ya nyaraka yake kubwa ambayo imeleta mchango mkubwa ni pamoja na waraka Leo Tomes

Kufikia hivi sasa  kanisa limetangaza madaktari wa kanisa 37 pekee.

Baba Leo wa 1 anafanana kwa ukaribu baadhi ya mambo na Baba Leo 14. Wote ni waatalam wa sheria na ni watu waliojitoa wakati wa majanga au shida.

Leo 1 alijitoa sana kwa masikini, hata nyakati za magonjwa na majanga alikuwa mstari wa mbele. Ndiye papa aliyekaribisha wakimbizi wengi na kuhudumia wagonjwa.

Leo wa 14 wakati wa corona, alionekana akitembeza sakramenti ya ekaristi hadharani nyakati ambazo kila mtu alijufungia ndani huko Peru. Hata nyakati za mafuriko alijitokeza kusadia wahanga wa majanga mbalimbali

Pope Leo 1 alikuwa mmoja kati ya magwiji wa sheria za kanisa na za kiraia ambapo alifaninikiwa kusuluhisha migogoro mikubwa mno kabla na baada ya kuwa Papa.

Papa Sixtus III aliwahi kumtuma kutatua mgogoro wa Aëtius, Kamanda wa Kirumi huko Gaul, na Hakimu wa Albinus. Baada ya kufanikiwa kuwapatanisha alipewa heshima kubwa sana kwa kanisa.

Baadae Baba Mtakatifu Zosimus nae alimpa jukumu la kutatua mgogoro wa uongozi kwa kanisa la Gallican ambalo lilikataa kuutambua Uongozi wa Kanisa la Roma.

Alikuwa Papa aliyenyooka sana, mwaka 446 aliwaandikia barua makuhani wa kanisa la Muaritania Africa kuwaonya kuhusu kufuata miiko na sheria za kanisa katoliki.

Papa Leo 1 ni mbobevu wa sheria za kanisa akiwa na PhD. Pengine ubobevu wa sheria wa Leo 1 ndio umemfanya Leo 14 kuchukua jina  la Leo the Great ambaye alibobea kwenye sekta hiyo pia.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG