BANDA MEDIA BLOG

VIONGOZI WA KITAIFA WAOMBEWA JIMBONI KWA SIMBACHAWENE.

NA MWANDISHI WETU, MPWAPWA

 MEI 18, 2025 imefanyika ibada ya maombezi kwa ajili Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake katika serikali ya awamu ya 6  pamoja na jamii kwa ujumla ikizingatiwa nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu.

 Mgeni Maalum katika maombi hayo alikuwa Mbunge wa Jimbo la  kibakwe George Simbachawene aliyewawakilisha Viongozi engine kutokana na nafasi yake ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu na utawara Bora.

 Viongozi wa Dini walioongoza maombi hayo wamesisitiza kuwa wananchi wa Tanzania hasa wa Jimbo la Kibakwe kwenda safari Moja na  Simbachawene pamoja na Dkt Samia Suluhu Hassan na hasa ikizingatiwa Ushirikiano wao WA kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo hilo

Mbali na hivyo viongozi hao wameomba amani iliyopo isichezewe kwani ni nadra sana kuirudisha ikipotea,Umoja huo wa madhehebu ya Kiskristo na Kiislamu unaoundwa na madhehebu  9 lengo lao likiwa ni kuwaombea viongozi wa kitaifa kila wakati ili nchi inlendelee kuwa na amani ya kudumu.

    Kwa upande wa diwani wa Kata ya Pwaga Wille Mgonela ambaye ndiye muandaaji wa maombi hayo mbali na kusisitiza amani lakini ametoa Rai kwa wananchi wa kata ya Pwaga na maeneo mengine kujiandikisha katika daftari la wapiga kura linaloendelea wakati huu kwa kipindi cha awamu ya pili, ambapo Diwani huyo pia alimuomba Waziri Simbachawene aweze kukamilisha mradi wa maji unaojengwa katika kata yake wenye kubeba Lita laki tano za maji ambazo zinatosheleza kuwahudumia wananchi wa kata hiyo huku zoezi la usambazi wa huduma hiyo ukiendelea kuboreshwa zaidi ambapo ukishakamilika utaweza kuwahudumia wananchi hao bila ya bughudha yoyote.

    nae Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi Mgutho Mathew ambaye ndiye msemaji wa Chama ngazi ya wilaya amepongeza jitihada zinazofanywa kwa ushirikiano wa Mbunge na Diwani kwa kutekeleza ilani ya CCM, ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Kibakwe.

 Pia Mwenezi Mgutho amewashauri wananchi kuendelea kuwaamini  madiwani, mbunge  pamoja na Rais kwa kazi nzuri wanayoifanya ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi lakini pia hakusita kuwashukuru viongozi wa dini kwa kuweka UTARATIBU wa kufanya maombi kwaajili ya taifa na kulinda amani ya Nchi ambayo ni tunu iliyoachwa na waasisi wa taifa letu

    Mbunge wa Jimbo la Kibakwe George Simbachawene kwa akiongea amekiri kuwa katika Jimbo lake analoliongoza kwa kushirikiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hasani wametekeleza ilani kwa asilimia kubwa sana ambapo katika Kila kata amegusa miradi mikubwa yenye faida kwa wananchi wote kma vile:

    1:Uboreshaji wa huduma ya Afya kwa kujenga vituo vya afya katika kata ya Ipera,Rudi,Mtera, Kibakwe, Pwaga, Chipogoro,Wotta pamoja na muendelezo wa ujenzi wa kituo cha Afya Kata ya Mbuga pamoja na Mlunduzi ambapo ujenzi wake unaelekea kuanza muda sio mrefu kwani fedha zake tayari zimeshapatikana

   2:Upande wa elimu mheshimiwa Simbachawene amesema kuwa ameboresha miundombinu ya madarasa pamoja na kuzifanya baadhi ya shule za Sekondari kuwa high school ikiwemo shule ya Sekondari ya Mtera,lakini amesema kuwa kwa sasa Kila kata zipo shule zenye madarasa ya kisasa na walimu wa kujtosheleza lengo likiwa ni kukuza ufaulu wa watoto wa Shule hizo za msingi na sekondari

   3: Katika upande wa Umeme kwenye kata za Jimbo lake 18 maeneo yote tayari yamefikiwa na umeme na yote tayari yapo katika matumizi ya umeme kwa ufasaha

   4:Ujenzi wa mahakama ya mwanzo ya kisasa katika kata ya Ipera lengo likiwa ni kupunguza adha wanayokutana wananchi wake wanapohitaji huduma za kisheria

    Mbali na hivyo Mheshimiwa Simbachawene amesema kuwa yapo mambo mengi sana ambayo ameyafanya katika Jimbo hili ambalo Kila mtu ni shahidi wa yaliyofanyika ambapo ameomba wananchi waendelee kumpa muda zaidi ili aweze kumalizia yake machache ambayo yamebakia,Lakini pia Mheshimiwa Simbachawene amegusia ujenzi wa barabara ya kutoka Kongwa-Mpwapwa amekiri kuwa tayari mkandarasi yupo site tayari kwa ujenzi mara ambapo amesema UTARATIBU wa kumpata mkandarasi kwaajili ya barabara ya Mpwapwa-Kibakwe fedha ipo ambacho bado kinafanyiwa kazi kwa sasa ni upatikanaji wa mkandarasi ambae atajenga barabara hiyo ya kutoka Mpwapwa-Kibakwe mara baada ya ujenzi wa barabara ya Mpwapwa -kibakwe zoezi litakalo fuata ni barabara ya Kibakwe-Chipogoro,Amesema

    Yapo mengi sana tumefanya kwa kushirikiana na Waheshimiwa wenzangu madiwani lakini pia shukrani za dhati nizipeleke kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwani yeye ndie anaeidhinisha fedha hizi ziweze kuja kwenye miradi na ndio maana nimefanya mambo mengi na makubwa sana katika Jimbo hili la Kibakwe na mambo mengine makubwa yatazidi kuja kulingana na mipango niliyo nayo katika kutekeleza vyema ilani ya Chama Cha Mapinduzi,  kwa kumalizia kifungu cha biblia "Wakorosai 4:2 (Dumuni katika kuomba)

(Kesheni katika kuomba)

(Huku mkishukuru) Amesema Mheshimiwa Simbachawene 




 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG