BABATI:
Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Fredrick Sumaye amesema Rais Samia Suluhu Hassan amefungua milango ya kidiplomasia ambayo imechangia ushirikiano mzuri na mataifa mengine na kuchangia ongezeko la wawekezaji kutoka nje ambao wamewekeza katika sekta mbalimbali.
Sumaye ameeleza hayo leo Juni 4,alipopata nafasi ya kusalimia wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mollel Papaa Wilaya ya
Babati mkoani Manyara katika ziara ya Katibu wa NEC itikadi Uenezi na Mafunzo
wa CCM, Amos Makalla katika mikoa ya kaskazini.
Pia
amesema Rais Samia amedumisha utulivu na amani katika nchi kwa kurudisha
amani kwa wafanyabiashara wa ndani ambayo imekuwa ni moja ya kivutio kwa
wawekezaji wengine kutoka nje.
Aidha, alisema hapo awali wafanyabiashara
walifunga biashara zao na kupoteza matumaini lakini Rais Samia alirudisha
utulivu amani na matumaini kwa watanzania na pia watanzania walikuwa
wamefungiwa milango katika nchi za nje lakini Rais Samia alifungua milango ga
kidiplomasia.
“Rais Samia alifungua milango ga kidiplomasia ya nje leo wageni wamejaa, watalii na wawekezaji wanaimani na Tanzania na wanakuja kwa wingi kuwekeza katika nchi yetu na watanzania tunaombwa tushirikiane nao kama ikiwezekana, mama Samia amefanya kazi kubwa sana kurudisha ushirikiano wa kimataifa,” amesema Sumaye.





