BANDA MEDIA BLOG

POLEPOLE AJIUZULU NAFASI ZAKE ZA UONGOZI- MAKALA AKILI KUIONA BARUA YAKE MTANDAONI

 

Balozi Humphrey Polepole Ajiuzulu
Balozi Humphrey Polepole Ajiuzulu

"Kwa heshima na unyenyekevu naomba kukutaarifu (Rais Samia Suluhu Hassan) kuwa nimefikia uamuzi wa kujiuzulu nafasi yangu ya uongozi wa umma nikiwa Balozi na Mkuu wa kituo cha uwakilishi wa Tanzania Havana Cuba.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha mapinduzi CCM, CPA Amosi Makala akijibu maswali ya waandishi wa habari amekili kuiona barua hiyo ikisambaa mtandaoni " mwenye kuthibitisha kuwa barua hiyo ni ya kweli ni yeye mwenyewe, lakini nimefurahishwa na alivyomalizia kusema yeye badoni mwanachama wa CCM", amesema

Sehemu ya Baurua ya Polepole, imesema Uamuzi huu sio mwepesi bali umetokana na takafari ya kina juu ya mwenendo wa uongozi katika nchi yetu. Uzoefu wangu kama Mbunge na hatimaye kama Balozi.

Mhe. Rais nilipokea kwa heshima kubwa uteuzi na dhamana uliyonipa kuwa mwakilishi wa nchi yetu katika ngazi ya Kimataifa, niliamini na ninaendelea kuamini lilikuwepo kusudi na kazi muhimu ya kuyashika, kuyasimika, kuyasimamia, kuyaimarisha na kuyaendeleza maslahi mapana ya nchi yetu katika maeneo ya uwakilishi uliyonipa dhamana ya kuyasimamia. Ni heshima kubwa na isiyopimika kuaminiwa kuwa mwakilishi wako, nchi yetu, Taifa letu, wananchi na Mamlaka ya nchi. Kwa hili nasema ahsante.

Hata hivyo kwa muda wote wa kuhudumu ndani na nje ya nchi, nimefuatilia kwa karibu na kushuhudia kwa masikitiko makubwa mwelekeo wa uongozi usiojielekeza ipasavyo katika kusimamia haki za watu, amani na kuheshimu watu, kufifia kwa dhamira ya kweli na uwajibikaji wa dhati wa kushughulikia kero na changamoto zao na kudidimia kwa maadili ya uongozi katika ngazi mbalimbali. Kudhohofika kwa utekelezaji wa majukumu ya msingi ya serikali kwaajili ya ustawi wa wananchi- mambo haya yanateteresha maslahi mapana ya Tanzania, haya yote yamezidi kunifanya nikose amani ya moyo na imani katika uongozi niliopo ndani yake sasa.

Matukio ya hivi karibuni ya wazi ya kukiuka misingi, utamaduni na desturi ya Chama Cha Mapinduzi hususan katika mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya Chama ambao kwa kila awamu huwa ni msingi wa kukihuisha Chama na fursa ya kufanya mageuzi ambayo kwa pamoja hukipa chama sura ng'aavu mbele ya umma kabla ya uchaguzi; desturi hii ya kufanya mageuzi ndani ya chama imekuwa nguzo muhimu ya ukubalifu na ushindi wa CCM mbele ya Umma. Imekuwepo kauli maarufu ya CCM isemayo "Chama kwanza mtu baadaye", mwanzoni mwa mwaka huu nilipoona kauli hii inafanyika vinginevyo, nimejiuliza mara kadhaa ni maslahi ya nani yanayopiganiwa wakati huu, mtu, kikundi au Chama Taasisi?"- Balozi Humphrey Polepole

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG