Haki na waji ndiyo Umekuwa msingi wa Kikao kazi hicho..
Kaimu Aflisa Tawala mkuu wa jiji la Dar es salaam Flora Mgonja ,amewaambia waajiri kuwa wana jukumu la kuweka mazingira bora ya kazi ili wafanyakazi wajione wapo mahali salama ili kufanya kazi ya kujenga Taifa kwa bidii.
Amesema waajiri katika mamlaka na Taasisi mbalimbali wanatakiwa kuwakumbusha maafisa utumishi na wakurugenzi umuhimu wa kuwasiliana na kuwafahamu watumishi wao ili kutambua changamoto wanazokabiliana nazo.
Ameongeza kusema kuwa kuna baadhi ya watumishi wanachukia ajira zao kutokana na mahusiano mabaya na wakuu wao wa kazi. Hivyo amezitaka pande zote kuboresha mahusiano kazini ili kwa pamoja waweze kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa Wananchi.
Aidha ameipongeza TALGWU kwa namna ambavyo inafanya kazi na Waajiri na kusema mpango huu wa kukutana na waajiri una tija kwa maslahi ya Wafanyakazi nchini.















