BANDA MEDIA BLOG

MAANDALIZI KAMILI CCM: DKT SAMIA NA NCHIMBI KUCHUKUA FOMU INEC KESHO

             


                     

Dodoma

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka mikakati maalum kwa ajili ya zoezi la kesho Jumamosi, ambapo mgombea urais wake, Dkt Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgombea mwenza, Dkt John Nchimbi, watakwenda rasmi katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuchukua fomu za kugombea nafasi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini note. 

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amesema maandalizi yote yamekamilika na baada ya kuchukua fomu, wagombea hao wataelekea makao makuu ya CCM kuzungumza na wanahabari pamoja na wanaccm kuhusu hatua hiyo muhimu kuelekea uchaguzi mkuu.

“Baada ya wagombea wetu kuchukua fomu, watafika katika ofisi hizi za Chama hapa makao makuu na kuzungumza nanyi,” alisema CPA Makalla.

Pamoja na kutoa taarifa hiyo, Makalla amewataka Watanzania kuendelea kuiunga mkono timu ya Taifa ya soka, Taifa Stars, inayoshiriki michuano ya CHAN inayoendelea katika nchi tatu za Afrika Mashariki. Kenya, Uganda na Tanzania ambapo amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Sukuhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa akinitoa na kuiunga mkono time ya Taifa Taifa Stars. 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG