BANDA MEDIA BLOG

AMANI HAIJI KWA MTUTU WA BUNDUKI WALA KWA MATAMKO-ASKOFU CHILONGANI

 NA MWANDISHI WETU, DODOMA

"Juzi juzi Imesheherekewa, miaka 64 ya Uhuru japo kwa hofu,  wakisoma historia ya Tanzania tarehe 9 Desemba 1961 Mwalimu Nyerere aliposimama kuwatangazia watanzania kwamba: *“Hatimaye, Tanganyika nchi yenu muipendayo sasa iko huru milele”,* habari hii njema ilipokelewa kwa vifijo na shangwe nchi nzima, watu walikusanyika wakiimba na kucheza, wengi wakaandamana wakiwa na bendera za TANU na matawi ya miti wakishangilia uhuru wao.

 "hebu fikiria Mungu anatawala hapa Tanzania kiasi kwamba askari polisi, JWTZ, FFU, Magereza, Uhamiaji, JKT, Mgambo, wote wanatupa silaha zao wanaungana na raia wanaimba mapambio wanasifu pamoja na raia*. Hiyo itakuwa ni nchi ya namna gani?", 

ASKOFU wa kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Central Tanganyika ( DCT) DKT. Dickson Chilongani ndiye Amesema hayo kwenye kanisa kuu la Roho Mtakatifu wakati akihubiri kwenye ibada ya Krismasi 2025 "pasi shaka baadhi ya wananchi wameingia kwenye Krismasi hii ya mwaka 2025 wakiwa na hofu ya maandamano. Hofu ya Risasi, hofu ya mabomu na Hofu ya Kufungiwa ndani kutokana na matishio yaliyokuwepo, "lakini nasema Amani iwe Nanyi kutokana na kuzaliwa kwa Yesu Kristo hii leo", amesema

Askofu akambusha akisema kama Mtu angetembea zile siku 3 zilizofuatia uchaguzi wa Octoba 29, mwaka huu  angeona jinsi majiji haya makubwa yalivyokuwa katika hali ya ukiwa – hakuna watu barabarani, hakuna milio ya magari, boda boda wala bajaji. Ni milio ya mitutu na mabomu ya machozi, Hali hiyo hawajawahi kuiona na hawatamani kuiona tena.

Dkt. Chilongani anasema imefika mahali rraiana polisi wanaogopana, huku  wahubiri kama yeye wanawaza watahubiri nini, kwani wakisema hivi watu watawaweka kwenye kundi fulani na wakisema hivi wataweka kwenye kundi hili. "Hata hapa mlipo mnajiuliza hivi Askofu atasema nini Ataishutumu serikali au atawakosoa waandamanaji, si kazi yangu kuhukumu, hukumu ni ya Mungu peke yake", amesma

Aidha Chilongani akatoa ushauri huu, kuwa Wasipoteze muda katika kushutumiana na kulaumiana, na kwamba Wakitaka taifa lao liwe na amani ya kweli, ni lazima wamtangulize Mungu, ni lazima wamwombe aingilie kati, ni lazima wampe nafasi amiliki, awe mtawala wa taifa lao: atawale akili za vijana wao, atawale mioyo ya viongozi wao, atawale mioyo ya askari wao, atawale mioyo yao. Hapo ndipo watashuhudia amani ya kweli 

Pia walinzi wa nchi ndio wanakiwa kuwa kwanza kushuhudiwa habari njema na kupokea wokovu na kuanza kuimba kwa furaha na shangwe nino Amani. Kuna wakati huwa anaona kama tumewasahau walinzi kwani Nchi nyingi za Ulaya na zinazotuzunguka zina machaplain wanaoongoza ibada majeshini na kuwahubiria askari,  Hii inasaidia sana kuimarisha amani ya nchi. Wao hapa Tanzania hawana  machaplain majeshini. *Je askari wao hawamhitaji Mungu?* Mbona kila wakati wanaabudu nao makanisani?  Anaesema na kuhoji

Mwisho, Mhashamu Askofu Dkt Chilongani, akawataka Wakristo wakumbuke kwamba wao wakristo wanapaswa kuwa mfano katika kutafuta amani, kama Nabii Isaya katika 9:6 anavyowakumbusha kwamba huyu anayezaliwa ni mfalme wa amani. Katika Warumi 12:18 Mtume Paulo anawahimiza akisema: Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.Mwandishi wa Waebrania 12:14 anasema: Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hapana mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao. Akasema *Amani na utakatifu vinakwenda pamoja*. Mtu hawezi sema ameokoka anampenda Mungu wakati huo huo matendo yake yanasababisha uvunjifu wa amani. Yesu mwenyewe katika Yohana 14:27 anasema: Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. 

"Amani haiji kwa mtutu, wala haiji kwa matamko, Amani inakuja kwa kumwamini Yesu, kwa maombi, kwa mazungumzo na matendo mema", amesema

Akamaliza kwa kuwatakia Wakristo wote *Heri ya Christmas* 

🌲🌲🌲🌲🌲🌲🌲🌲

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG