*AYOUB MOHAMMED MAHMOUD ATOA WITO WA MASHIRIKIANO K
Katika kikao cha Baraza la Kawaida la kikanuni la UWT Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja kilichofanyika Tarehe 21/12/2025 katika Tawi la CCM Chaani Masingini, MhlOHAMED ametoa wito mzito kwa wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Wilayani humo kuwataka wote kudumisha amani, mshikamano na mashirikiano.
Akizungumza mbele ya wajumbe wa kikao hicho, Mhe. Ayoub Malieleza kuwa mivutano inayojitokeza mara kwa mara katika jumuia mara nyingi husababishwa na ukosefu wa mawasiliano. Alisisitiza kuwa mivutano hiyo inaweza kuepukika endapo kutakuwepo na utamaduni wa kusikilizana na kuheshimiana.
“Mivutano haiwezi kuisha kabisa, lakini inaweza kudhibitiwa kwa njia ya mazungumzo ya wazi na mashirikiano ya kweli,” alisema Mhe. Ayoub. “Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunafanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya Jumuiya na maendeleo ya jamii.”
Aidha, aliwahimiza viongozi na wanachama wa kikao hicho kuimarisha mashirikiano katika Jumuia na kuleta maendeleo endelevu na kuimarisha umoja.
#WanawakeJeshiDktSamianaDkMwinyi #KazinaUtuTunasongambele



