BANDA MEDIA BLOG

KIONGOZI NCHINI IRAN - WAANDAMANAJI WANAJARIBU KUMFURAHISHA TRUMP

 .

Chanzo cha picha,Reuters

Akizungumza na wafuasi wake mapema asubuhi ya leo, Khamenei aliwapuuza waandamanaji na kuwaita "kundi la waharibifu" wanaotaka "kumfurahisha" Rais wa Marekani Donald Trump.

Katika hotuba ya video iliyotangazwa kwenye televisheni ya kitaifa, Khamenei alisema: "Kundi la waharibifu lilijitokeza Tehran na maeneo mengine na kuharibu majengo ya nchi yao ili kumfurahisha rais wa Marekani."

"Hiyo ni kwa sababu alitoa madai ya kipuuzi kwamba anawaunga mkono ninyi waandamanaji na watu ambao ni hatari kwa nchi. Kama ana uwezo, anapaswa kuendesha nchi yake mwenyewe."

Iran imetuma barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiilaumu Marekani kwa kuyageuza maandamano hayo kuwa kile ilichokiita "vitendo vya uasi na uharibifu ulioenea" huku Trump naye akisema Iran iko "katika matatizo makubwa".

Kiongozi huyo wa Iran, ambaye amekuwa madarakani tangu 1989, aliongeza kwamba mikono ya Trump "ina madoa ya damu ya zaidi ya Wairani elfu moja waliouawa wakati wa vita vya siku 12 [na Israeli]".

"Kundi la watu wasio na uzoefu na wasiojali wanamwamini na kutenda kulingana na matakwa yake. Wanachoma mapipa ya takataka ili kumfurahisha," anaongeza.

"Kila mtu ajue kwamba Jamhuri ya Kiislamu iliingia madarakani kupitia damu ya watu mia kadhaa wenye heshima na haitarudi nyuma mbele ya wale wanaokana hili."

Trump amekuwa mpinzani mkubwa wa utawala wa Iran kwa muda mrefu na aliahidi kuingilia kati ikiwa raia watauawa katika maandamano hayo

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG