MCHUNGAJI Robert Lumbasi wa Nchini Kenya amesema alikuja Tanzania mwaka 2023 kumtolea mahari, Malikia wa Nyimbo za Injili Rose Muhando ambaye kwa sasa amefikisha umri wa miaka (50) ambapo tukio hilo lilifanyika kifamilia zaidi na watu wa karibu kuhudhuria.
Mchungaji huyo ambaye kwa sasa ni Askofu akiwa kanisani kwake amewaeleza wanaume walitambue hilo kuwa mwimbaji huyo maarufu wa njimbo za injili hayupo single. (SOKONI) akama alivyotamka na kuwafanya waumini kuangua 
Aidha, mchungaji huyo amesema anampenda sana na kumheshimu Rose hivyo Kwa pamoja wataipeleka injili mbali zaidi
Ukiacha hayo, kipindi cha nyuma Rose Muhando alisema hajawahi kuolewa ingawa anajivunia kuwa na watoto watatu na kuwalea mwenyewe vizuri pamoja na kuwasomesha hadi vyuo vikuu kwa juhudi zake za kufanya kazi kwa bidii pasipo kutegemea mwanaume
Rose kwa wakati huo alisema ndoa sio kitu kibaya kwake ila hana haraka ya kutaka kuolewa na yeyote, akipata mwanaume wa kumuoa lazima aangalie nini ataleta katika maisha yake , je mwanaume yupo katika hatua nzuri kiuchumi kuweza kusimamia kama kiongozi wa familia kutimiza majukumu yake , na upendo anao? Ni vitu ambayo Rose alisema anavingalia Kwa mwanaume wa kuwa nae katika ndoa.

