BANDA MEDIA BLOG

RAIS WA COLOMBIA AMJIBU VIKALI TRUMP.

 

Rais wa Colombia, Gustavo Petro, amemjibu vikali Donald Trump baada ya kutishiwa kutiwa mbaroni na kuitwa muuza dawa za kulevya, huku Trump akidokeza uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Colombia kama ilivyotokea Venezuela.

Petro, ambaye ni mwanasiasa wa mrengo wa kushoto na aliwahi kuwa mpiganaji wa msituni, amesema wazi:

 “Sijawahi kuwa muuza madawa. Mali yangu ni nyumba ya familia ninayoendelea kuilipia kwa mshahara wangu. Akaunti zangu za benki ziko wazi kwa umma."

Kisha akaongeza kwa tahadhari kali:

“Ukinikamata, utachochea ‘Jaguar wa Watu’. Niliapa kutotumia silaha tena tangu Mkataba wa Amani wa 1989, lakini kwa ajili ya Taifa langu, nipo tayari kuishika tena.”

Petro pia amewaonya wanajeshi wa Colombia kwamba yeyote anayeipa Marekani uzito kuliko bendera ya Colombia, ajiuzulu mara moja.

Amesisitiza kazi yao ni kuwalinda wananchi na kupambana na mvamizi yeyote.

Petro ameweka wazi msimamo wake dhidi ya uvamizi wa Marekani, akiamini kuwa Trump hatathubutu kumgeukia kiongozi mwenye uungwaji mkono wa wananchi na historia ya mapambano.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG