BANDA MEDIA BLOG

REFA BOUBOU TRAORE' KUTOKA MALI ALIVYOUZA UTU NA HESHIMA YAKE MBELE YA ULIMWENGU, AFCON TAIFASTARS VS MOROCCO

Nianze kwa kuipongeza timu ya Tanzania - TaifaStars na benchi la Ufundi chini ya Master Miguel Ángel Gamondi kwa mbinu mujarabu walizokuja nazo kwenye mchezo wao dhidi ya Morocco (mwenyeji) hakika tumeshuhudia ufundi wa viwango vya hadhi ya NYOTA 5 pale nyuma ule ukuta ni zaidi ya ukuta wa Yeriko naweza kusema Mashujaa wetu walikuwa kwenye FORM haswaa kila mchezaji amedeliver.

Zile takwimu za kipindi cha kwanza Morocco wanatoka bila SHOT ON TARGET haikuwa bahati mbaya bali ni akili kubwa ya Master Gamondi alivyokuwa ameusuka ukuta na morali ya Wachezaji ambao leo wamecheza DO or DIE (kizalendo kabisaaa! kwa kuipambania bendera ya Tz) na ndiyo sababu ya Morocco kukosa maarifa ya kuifungua ile ngome ya Coprol Baka, Mwamnyeto, Job na kule kati Miroshi na Mabula wamepiga kazi chafu iliyowaduwaza Morocco ambao hawakuamini macho yao kama wanatoka bila goli hata pale zilipoongezwa dk 7 nzima kipindi cha kwanza bado ilikuwa hola hola.
Nakubali Morocco wametuzidi uwezo kwa kila kitu kwenye soka lakini bado wakaamua kuweka planB ya mchezaji wa 12 (REFA) ambaye kwa hakika ameiamua mechi huenda kama si yeye basi hadithi ingekuwa tofauti TaifaStars ingeishangaza CAF na Morocco ambao waliingia na matokeo uwanjani kabla ya game.
Tangu mwanzo mchezo unaanza Mwamuzi wa kati Boubou Traore alionekana tayari amechagua upande maana yapo maamuzi ya madhambi waliyokuwa wanafanya wachezaji wq Morocco Traore' alivaa miwani ya mbao ikawa TaifaStars wakifanya hata zile faulo nyepesi dhidi ya Wamorocco Mwamuzi alifoka na wakati mwingine adhabu ya kadi ya njano ilikuwa suluhu as if kadi za njano ni za TaifaStars tu🤣. Hata hivyo maamuzi yake hayakuwatoa Stars mchezoni waliendelea kupambana hadi tone la mwisho na kutoruhusu makosa ya kutoa mwanya wa hujuma za Mwamuzi.
Dakika za lala salama 93+ ikisalia dk 1 mchezo uishe Mwenyezi Mungu akaamua kumdharirisha Mwamuzi Boubou Traore' kwa kuipatia TaifaStars nafasi ya penati ambayo ni ya wazi haihitaji VAR wala mjadala maana hata Brahim Diaz wa RealMadrid aliyetusulubu kwa goli 1, alistuka na kuweka mikono kichwani akijua tayari Tanzania imepata tuta kifuatacho ni kusawazisha au kipa wao Yassine Bounou afanye maajabu ya Diara wa Mali na hata wachezaji wa Morocco kiakili walishakubali ni penati kwa kosa la kushikwa na kusukumwa Iddi Nado na leftback wao. Lakini kilichotokea ni Mwamuzi kujitoa ufahamu mbele ya Dunia ya wapenda soka kwa kuwanyima penati TaifaStars ambao ilikuwa golden chance ya kuswazisha na kwenda kwenye MATUTA kama kwenye game ya Mali vs Tunisia.

Afrika bado safari ni ndefu hata tuweke teknojia kiasi gani maana Boubou Traore' kaikataa hata VAR isiyobagua isiyopendelea isiyoangalia status ya taifa ni ajabu VAR mwamuzi wa HAKI na mtoa shaka kwenye maamuzi amegomewa na Boubbou hata Stars waliposhinikiza jamaa aligoma na kuamua kuinajisi taaluma, heshima na utu wake akautoa kwa kuivusha Morocco hatua ya Robo Fainali.
Nachelea kusema Mwamuzi amenunuliwa au alipewa maelekezo mahususi ya kuhakikisha Morocco anafuzu na hii ni ishara ya CAF kuwekwa mfukoni mwa Morocco maana sio kwenye AFCON wala CAFCL wala kombe la Shirikisho uamuzi unakuwa tata ni kweli wamewekeza kwenye soka kuanzia miundombinu hadi timu zao za Taifa na hata vilabu vyao vina ukwasi vinasajili mawe hasa lakini soka lina matokeo matatu wakati mwingine bahati huamua mechi leo wameikatili hadi bahati ya Stars licha ya ubora wao.
Haya nisiwachoshe! 🤣 binafsi naona Gamondi aachiwe timu hadi AFCON ya 2027, huenda tukaibeba EAC kama tulivyoibeba baada ya majirani kuaga kwenye makundi na wengine wakishindwa kufuzu.
Wasalaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG