Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imegawa pikipiki 2016 vifaa vya upimaji wa ubora wa maji pamoja na vifaa vya uunganishaji na ukarabati wa mabomba ya maji vijijini kwa Vyombo vya Utoaji Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) 88 katika iliyofanyika jijini Dodoma leo Januari 22, 2026.
Hafla hiyo fupi ya kugawa nyezo hizo ilihudhuriwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), Katibu Mkuu hiyo, Mha. Mwajuma Waziri, Memejimenti ya Wizara na RUWASA pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya maji.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Aweso amesisitiza kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama, ambapo ameagiza tathmini ifanyike kwa vijiji 1,575 ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya maji ili navyo viweze kufikiwa ifikapo 2030.
Naye Katibu Mkuu wa hiyo, Mha. Mwajuma Waziri amewahimiza mafundi (technicians) na watendaji wa CBWSOs kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia utaalamu ili kuhakikisha huduma bora na endelevu ya maji inatolewa kwa wananchi waishio vijijini.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA, Mha. Wolta Kirita alisema kuwa, Wizara ya Maji kupitia programu ya PforR inayotekelezwa na RUWASA imefanikisha ununuzi wa pikipiki 216, seti 86 za vifaa vya kupima ubora wa maji pamoja na seti 128 za vifaa vinavyotumika katika uunganishaji na ukarabati wa mabomba ya maji.
Alisema vifaa hivyo vitasaidia kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya maji vijijini na kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa CBWSO katika kuwahudumia wananchi wa vijijini huku akitoa wa watumishi wa taasisi hiyo kuzidi kufanya kazi kwa bidii na weledi.









