
Rahma Khamis Maelezo.
Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe Hassan Khamis Hafidh amesema Serikali ya Awamu ya nane ipo tayari kushirikiana na vyama vya ushirika ili kuwainua kiuchumi
Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Umoja wa Washirika wa Uchukuzi Bandarini Wilaya ya Mjini katika ziara kutembela Taasisi zilizomo katika Wizara yake na kujitambulisha
Amesema kuwa vyama vya Ushirika vina Mchango mkubwa katika kukuza Uchumi hivyo Serikali itaunga mkono juhudi zinazofanywa na vyama hivyo ili kufikia lengo lililokusudiwa
Amesema kuwa Kuwepo wa vyama hivyo kunasaidia kujikomboa kiuchumi na kuinua kipato Cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla
Naibu Waziri amefahamisha kuwa Serikali ina jukumu la kuhakikisha vyama vya ushirika vinafanya kazi kwa kufuata taratibu ili kuondoa umasikini
Aidha amevitaka vyama hivyo kuacha kulumbana na badala yake kushirikiana katika kazi kwa maslahi yao sambamba na kuwekeza katika taasisi ili kufikia malengo
Mwenyekiti wa Umoja wa Ushirika wa Wachukuzi Bandarini (UWABAZA) Masuod Haji Juma ameiomba a Wizara kupatiwa elimu ya utunzaji wa Fedha kwa wahasibu kwani wanahitaji uwazi katika ukusanyaji wa mapato
Wakitoa malalamiko yao wanachama wa vyama hivyo wameomba kupatiwa malipo kwa wakati ili kujikimu kimaisha na kuondosha malalamiko kwa baadhi ya wafanyakazi
Katika ziara hiyo Naibu Hafidh ameltembelea vyama mbalimbali vya Ushirika ikiwemo Sacoss zote bandarini,Boat Boys Syndicate Bandarini, Tax Service Bandarini,Tax Saccos Office na Muungano wa Umoja wa vyama vya Ushirika Kikwajuni.