BANDA MEDIA BLOG

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO KUANZA KUTUMIKA JUNE MWAKA HUU.

 

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato kukamilika Juni, 2026

Moshi mweupe wa matumaini umeanza  kufuka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato Jijini Dodoma baada ya Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa kueleza kuwa ndege zitaanza kuruka na kutua kuanzia Juni mwaka huu.

Uwanja huo kwa sasa umefikia asilimia 75.9, ukihusisha kazi mbalimbali ikiwemo barabara ya kuruka na kutua ndege. Kazi hiyo imefikia asilimia 99 na jengo la abiria limefikia asilimia 99.

Aidha, wakazi wanaozunguka mradi huo wameipongeza Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kukamilisha mradi huo na wananufaika  na fursa mbalimbali ikwemo  ajira.



Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG