Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi, Ndg. Kadari Singo, akiwasilisha mada kuhusu Uongozi wa kimkakati katika Uendeshaji wa Shughuli za Bunge wakati wa mafunzo kwa Kamati ya Uongozi, Tume ya Utumishi wa Bunge na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanyika leo tarehe 17 Februari, 2026 katika Ofisi ndogo za Bunge, Tunguu-Zanzibar.
Mafunzo hayo ya siku tatu (3) yameendelea leo tarehe 17 na yanategemewa kuhitimishwa kesho tarehe 18 Februari, 2026.
Viongozi mbalimbali wa Bunge wameshiriki katika mafunzo hayo akiwemo Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Naibu Spika, l. Daniel Sillo na Katibu wa Bunge, Ndg. Baraka Leonard.







