BANDA MEDIA BLOG

KATIBU MKUU KIONGOZI AFUNGUA MKUTANO WA SITA WA e -GA JIJINI ARUSHA

 



Na Happy Lazaro,Arusha 

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka amewataka Maafisa Tehama nchini kusimamia matumizi ya teknolojia ili kuhakikisha inaleta maendeleo badala ya  uharibifu  .
Ameyasema hayo leo jijini Arusha  wakati akifungua kikao kazi cha sita cha Mamlaka ya serikali mtandao (e-GA) kinachofanyika kwa siku tatu katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC), Arusha, amesisitiza umuhimu wa teknolojia katika kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Amesema kuwa ,Tehama ni kipaumbele cha serikali na tayari serikali.imepiga hatua kubwa katika kurahisisha utoaji wa hudjma kwa wananchi hali ambayo imewezesha huduma  hizo kupatikana kwa wakati toafauti na  kipindi cha nyuma.
Amesema kuwa, Tanzania imeonyesha mafanikio makubwa sana  katika.sekta ya Tehama na kuweza kutambuliwa kimataifa 
Balozi Dkt Kusiluka amesema kuwa teknolojia ni chombo cha msingi cha kuhakikisha huduma za umma zinatolewa haraka, kwa uwazi, salama, rahisi na kwa gharama nafuu.
“Huduma za serikali zinapaswa kuwa bora na kupatikana kwa wakati unaofaa, na teknolojia ndiyo nyenzo inayoweza kutimiza hili,” amesema.
Kauli mbiu ya kikao ni “Huduma Bora za Umma Kupitia Teknolojia”, ikilenga malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Uchumi 2050, ambapo zaidi ya asilimia 80 ya huduma za serikali zinatarajiwa kufanikishwa kidijitali.”
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya serikali Mtandao  (e -GA), Mhandisi Benedict Ndomba, amesema serikali imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma za umma kupitia mifumo ya kidijitali.
Mkutano wa siku tatu umewaleta pamoja washiriki 400 kutoka sekta za umma na binafsi kujadili maendeleo, changamoto na mustakabali wa huduma za kidijitali serikalini.
“eGA imeimarisha usimamizi wa miradi ya TEHAMA serikalini, kuendeleza mtandao wa mawasiliano ya serikali, na kusimamia vituo vya kitaifa vya kuhifadhi data vinavyowezesha taasisi za umma kuendesha mifumo yao kwa usalama,” amesema Ndomba.
Amesema kuwa,pamoja na mafanikio  bado kuna changamoto kadhaa zinazopunguza
ufanisi wa utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao ambapo  baadhi ya changamoto hizo ni uhaba wa wataalamu wabobezi wa TEHAMA katika maeneo mbalimbali na kasi kubwa ya mabadiliko ya teknolojia yanayotokea duniani na kuhitaji Maafisa TEHAMA kujengewa uwezo mara kwa mara ili kukabiliana na mabadiliko hayo.
Aidha ametaja changamoto nyingine ni kutofanyika kwa vikao vya Kamati za TEHAMA za taasisi ‘ICT
Institutional Steering Committee’ kwa wakati kama inavyoelekezwa katika Sheria ya Serikali Mtandao, ambapo athari yake ni kuwepo kwa mifumo ya TEHAMA ndani ya Taasisi ambayo haijibu mahitaji ya Idara zote husika ndani ya Taasisi, hivyo kutokuwa na tija iliyokusudiwa..
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Toba Nguvila, amesema mkoa huo utaendelea kuwa kinara wa matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Amesema Arusha imekuwa mwenyeji wa mikutano ya kitaifa ya serikali kwa miaka sita mfululizo kutokana na miundombinu bora na utayari wa kuunga mkono mageuzi ya kidijitali.
“Serikali ya Mkoa wa Arusha itaendelea kutekeleza maelekezo ya kitaifa katika kuimarisha utawala wa kidijitali na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi,”amesema Nguvila.
Amesema kuwa, Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa wadau wakuu wa Serikali Mtandao na wamekuwa watumiaji
wazuri wa mifumo ya TEHAMA katika utendaji kazi wa wa kila siku na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha ameipongeza e-GA kwa jitihada zake za kutoa huduma mbalimbali za serikali
mtandao, ikiwemo kuunganisha mifumo ya TEHAMA Serikalini kupitia Mfumo wa
Ubadilishanaji Taarifa Serikalini (GovESB), ambao umeongeza ufanisi wa utendaji kazi, kupunguza gharama za uendeshaji na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
“Mkoa wa Arusha unaunga mkono kikamilifu jitihada za Serikali Mtandao kama sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga Serikali ya Kidijitali.”amesema Nguvila .
“Ni rai yangu kwa Taasisi zote za Umma zilizopo mkoani Arusha kuendelea kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao, ili Mkoa wetu uwe mfano bora na kinara wa matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma kwa wananchi.”amesema 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar (eGAZ), Said Seif, amesema ushirikiano kati ya serikali, taasisi za mawasiliano na wadau wa teknolojia unaendelea kuimarisha mageuzi ya kidijitali.
“Mageuzi ya kidijitali si chaguo bali ni hitaji la msingi katika maendeleo ya Taifa,Ushirikiano huu umewezesha usalama wa mifumo ya kidijitali, upatikanaji wa huduma za mtandao, na matumizi ya teknolojia bunifu kama loT,” amesema Seif.”amesema Seif.
Seif amesisitiza kuwa uongozi na uratibu imara wa taasisi za serikali mtandao ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo endelevu ya taifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG