BANDA MEDIA BLOG

KONGAMANO LA ANUWANI ZA MAKAZI NA TEKNOLOJIA ZA HUDUMA ZA POSTA LAFUNGULIWA JIJINI DSM


*Aliyosema  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dkt. Jabir Bakari.

# Uwepo wa anwani za makazi zilizoandaliwa vizuri ni msingi muhimu wa kukuza uchumi wa kidijitali.

#Anwani za Makazi huwezesha huduma mbalimbali kuwafikia wananchi kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.

#Matumizi sahihi ya anwani za makazi humsaidia mwananchi kutambulika anapoishi na kurahisisha upatikanaji wa huduma na bidhaa mbalimbali.

#Bila anwani za makazi, huwezi kuwa na uchumi wa kidijitali unaofanya kazi ipasavyo.

 #Kuna umuhimu wa kutunza miundombinu ya anwani za makazi ili kuwezesha utoaji wa huduma muhimu zikiwemo za usalama, afya na elimu.

#Wiki ya anwani za makazi inatarajiwa kuhitimishwa Februari 8, 2026, ikiwa na lengo la kuwahamasisha wananchi kujisajili na kutumia anwani za makazi ili kurahisisha biashara na huduma mbalimbali katika uchumi wa kidijitali.

#Mfumo wa uchumi wa kidijitali unahitaji uwepo wa anwani za Makazi ili uweze kufanya Kazi ipasavyo.

#Viongozi wa Serikali za Mitaa wapo hapa ili waweze kusaidia kuboresha anwani za makazi hasa kwa maeneo ambayo bado hayajafikiwa.

# Kongamano hili  litatusaidia kuhamasika na kufahamu umuhimu wa anwani za makazi, na kwa yale maeneo ambayo anwani hizo hazipo, viogozi wa Serikali za Mitaa watatusaidia kuziweka.

#Kongamano hili limejumuisha makundi mbalimbali wakiwemo watu wa UNCAF, mitandao ya simu na watu wa teknolojia mbalimbali. Hii imasaidia  tukitoka hapa tuwe na uelewa wa pamoja juu ya umuhimu wa anwani za makazi na ubunifu wa kiteknolojia.

#Tanzania tutaendelea kushirikiana na nchi mbalimbali katika bunifu za kiteknolojia hasa maendeleo ya Posta.

*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI -MAELEZO*








Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG