NA MWANDISHI WETU, DODOMA
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, amesema kuwa ndani ya siku 100 za Rais Samia,, sekta ya uchukuzi imepata mafanikio makubwa yaliyoimarisha reli, bandari, usafiri wa majini na anga, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Ameyasema hayo wakati Akizungumza na waandishi wa Habari Februari 1, 2026 katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jijini Dodoma, katika kutoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi za Rais samia ndani ya siku 100.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali imefufua na kuboresha Reli ya TAZARA, hatua itakayoongeza uwezo wa reli hiyo na kuimarisha biashara na nchi za Kusini mwa Afrika.
Aidha, amebainisha kuwa reli za ndani zinakamilisha upembuzi yakinifu, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza kujitegemea kifedha, na uendeshaji wa reli ya SGR na MGR unaendelea kwa mafanikio.
Pia ameongeza kuwa ujenzi wa reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza unaendelea, huku kipande cha Dar es Salaam hadi Dodoma tayari kikiwa kinatoa huduma kwa abiria na mizigo.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali imekamilisha maandalizi ya upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam na kuanza maandalizi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, huku miradi ya bandari katika Maziwa Makuu na ukanda wa Bahari ya Hindi ikiendelea.
Pia ameongeza kuwa meli mpya za mizigo na abiria zimeanza kutoa huduma, huku Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokoaji Ziwa Victoria kikiwa kimekamilika, na boti za uokoaji na huduma za afya zikitumika kulinda maisha ya wananchi.
Aidha, amebainisha kuwa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam unajumuisha ujenzi wa magati 10 na matenki 15 ya mafuta, hatua itakayoiwezesha kuhudumia shehena hadi tani milioni 50 kwa mwaka kutoka tani milioni 32 za sasa.
Aidha, amebainisha kuwa mapato ya bandari yameongezeka kutoka Shilingi trilioni 1.15 hadi trilioni 1.44, huku mapato ya Forodha (TRA) yakiwa Shilingi trilioni 8.256, ongezeko la trilioni 1.174, ikithibitisha kuwa maboresho haya yanaongeza mapato ya taifa.
Aidha, amebainisha kuwa mafanikio haya yameimarisha uunganishwaji wa Tanzania kikanda na kimataifa, kupunguza gharama za usafiri, kufungua masoko na kuongeza ajira.
Pia ameongeza kuwa maboresho ya bandari na forodha ni ushahidi wa juhudi za Serikali ya Rais Samia katika kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi, huku Tanzania ikijiimarisha kama kitovu cha uchukuzi na lojistiki Afrika Mashariki na Kati.
Tags
HABARI