BANDA MEDIA BLOG

MAMBO 10 YALIYOMTOFAUTISHA MSEMAJI WA M23 WILLY NGOMA NA VIONGOZI WENGINE


Haya ni mambo 10 yanayomtofautisha Willy Ngoma aliyekuwa Msemaji wa M23 na Viongozi wengine kama vile Sultani Makenga na Bertrand Bisimwa;
1. Majukumu; Willy Ngoma alifanya kazi ya Usemaji wa M23, wakati Sultani Makenga anafanya kazi kama kamanda Mkuu wa M23, yeye anasimamia operesheni zote za M23.
2. Utaratibu wa kimajukumu; Ngoma alikuwa anafanya kazi chini au alikuwa ana ripoti kwa Makenga.
3. Kisiasa vs Kijeshi; Bertrand Bisimwa ndo Msimamizi Mkuu wa masuala ya Kisiasa, wakati Ngoma alijikita zaidi kwenye Mawasiliano ya kijeshi Ndani ya Kundi la M23.
4. Kujitokeza mbele ya Umma; Willy Ngoma alikuwa anatokea na kuonekana sana kwenye vyombo vya habari, ukilinganisha na Makenga, yeye hujitokeza kimkakati na Mara chache sana yaani.
5. Mikakati vs Mawasiliano;Makenga ameboresha na kutoa uelekeo wa operesheni zote za kijeshi Ndani ya M23, Wakati huo Ngoma alitengeneza mikakati ya namna gani operesheni hizo ziwasilishwe kwa Umma, kwa maana ya Mawasiliano ya Kimkakati ya shughuli zote.
6. Vikwazo vya Kimataifa; Wote watatu wamekumbana na rungu la vikwazo vya kimataifa, lakini Ngoma ndio alikuwa analengwa zaidi sababu ndio alikuwa anaonekana zaidi na aina ya majukumu yake ya Usemaji.
7. Kucheza na akili za watu; Ngoma Mara zote amekuwa akiifanya M23 na matendo yake kuwa ya kiulinzi, kiusalama na kutetea haki za raia, wakati huo Bisimwa akijikita zaidi kwenye masuala ya kisiasa na majadiliano mbalimbali yenye faida kwao.
8. Uhusiano na vyombo vya habari; Ngoma alikuwa akijibu mashambulizi dhidi ya tuhuma kutoka upande wa FARDC na Serikali ya DRC kupitia vyombo vya habari. Alikuwa anazima propaganda na kubadili upepo.
9. Mamlaka na maagizo ya operesheni; Tofauti na Makenga, Ngoma hakuwa anatajwa sana kama “kichwa” kwenye mambo mengi yaliyohusu mikikati ya Kijeshi ya M23.
10. Madhara baada ya kifo; Kama ingetokea ameuawa Makenga, Shughuli za kijeshi za M23 zingeathirika zaidi, lakini kifo cha Ngoma kimeathiri eneo la Mawasiliano pamoja na Propaganda za M23.
👉🏻Ni nini maoni yako?

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG