BANDA MEDIA BLOG

MTOTO WA KIKE ASIZUIWE KUFANYA MICHEZO KWASABABU INAFURSA YA AJIRA DUNIA-THOBIAS SANGA AFISA MICHEZO NJOMBE DC

 


Wakati serikali ikiendelea na mchakato wa ujenzi wa shule za michezi na vituo vya kufua vipaji,Huko mkoani Njombe baadhi ya taasisi za elimu zimeanzisha programu za kuvumbua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi mashuleni ili kuzalisha wana michezo wa kutosha na ajira kupitia sekta hiyo ambayo imekuwa na fursa kubwa ulimwenguni.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku ya vipaji iliyoanzishwa katika sekondari ya wasichana ya Collagine Wilayani Njombe Makamu Mkuu wa Shule Lino Kaduma amesema wameamua kuja na programu hiyo ili kuinua vipaji vya wanafunzi shuleni kwao na kisha kuishauri serikali kuona namna ya kutoa elimu kwa walimu wa michezo ili waweze kufundisha vyema wanafunzi michezo mbalimbali,Mwl Kaduma amesema mbali na michezo kuwa ajira lakini endapo watoto hususani wa kike watashiriki michezo ina amsha akili za wanafunzi na kisha kuzitaka jamii kuhamasisha watoto kucheza ili kuimarisha ubongo kwa kuwa ni sehemu ya afya.

Awali Thobias Sanga ambae ni afisa michezo wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe ambae ni mgeni rasmi katika tukio hilo la Michezo Collagine Sekondari amesema jamii inatakiwa kuondokana na tabia ya kuzuia watoto hususani wakike kushiriki michezo na kwamba serikali inaendelea na uwekezaji wa miundombinu ya michezo ili kuzalisha wana michezo wa kutosha .

Aidha amegusia suala la maandalizi ya AFCON 2017 ambayo yanaendelea kwa nchi za Africa Mashariki kwamba yamekuja kwasababu serikali imeonyesha utayari kwenye michezo hivyo kila mzazi na shule zinajukumu la kuendeleza vipaji vya watoto ili miaka michache ijayo timu za taifa ziwe na wachezaji mahiri wa kutosha.

Kwa upande wake wake Grace Sanga Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka Sekondari ya Collagine ameeleza manufaa ya kuanzishwa kwa programu hiyo shuleni kwao kwamba imewafana kuimarisha miili na akili zao na kisha kutoa rai kwa jamii zinazokandamiza wanawake kwenye michezo kuacha kwasababu ni utajiri mkubwa kwasasa.

Nae Katibu mstaafu wa chama cha mpira mkoa wa Njombe Njorefa Hansi Luwanja ametumia fursa hiyo kusisitiza jamii kuwekeza kwenye vipaji vya vijana ili waweze kuja kuajiriwa na vipaji vyao

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG