BANDA MEDIA BLOG

WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO MAGOMENI WAFURAHIA MIKOPO YA SERIKALI

 


Na Abdala Sifi WMJJWM-Dar Es Salaam 

Wafanyabiashara ndogondogo katika soko la Magomeni mkoani Dar es Salaam, wameeleza kunufaika na Mikopo inayotolewa na Serikali kwa kusimamiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamiii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum kupitia Benki ya NMB.

Wameeleza hayo tarehe 26 Februari 2025 mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.John Jingu alipotembelea soko hilo kwa lengo la kuzungumza nao na kujionea namna walivyonufaika na mikopo inayotolewa na Serikali kupitia benki ya NMB ili kuwawezesha kuimarisha na kukuza biashara zao.

Katika ziara hiyo, Dkt. Jingu alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali na kusikiliza mafanikio ya wafanyabiashara hao. Alieleza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji wa mikopo kwa makundi maalum, hususan wanawake na vijana, ili kuongeza ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi wa kipato cha chini.

“Nimezunguka na kuwasikiliza wafanyabiashara ndogondogo hapa soko.    

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG