Na:
Ilikuwa ni mkutano wa kwanza kati ya pande hizo tangu Idara ya Hazina ya Marekani ilipoiwekea vikwazo Jeshi la Ulinzi la Rwanda na maafisa wanne wakuu Machi 2 mwaka huu.
Washington imeilaumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la waasi la M23 kwa kuendeleza vurugu hali mashariki mwa Kongo. Rwanda inakanusha kuiunga mkono M23. M23 ilifanya mashambulizi makali mashariki mwa Kongo mnamo Januari 2025 na bado inashikilia maeneo makubwa ya ardhi.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rwanda "zilikubaliana kwa mfululizo wa hatua zilizoratibiwa ili kupunguza mvutano na kuendeleza utulivu," kulingana na taarifa ya pamoja ya Marekani, Kongo na Rwanda iliyotolewa na idara ya serikali Jumatano.
Juhudi hizi zinajumuisha kujitolea kwa pande zote kwa hatua maalum za kuunga mkono uhuru wa kila mmoja na uadilifu wa eneo, kutengwa kwa vikosi na kuondolewa kwa hatua za kujilinda na Rwanda katika maeneo yaliyoainishwa katika eneo la DRC, juhudi zilizopangwa na zilizoimarishwa na DRC za kutuliza FDLR, na ulinzi wa raia wote.
Kundi la FDLR lilianzishwa na Wahutu waliokimbia Rwanda baada ya kushiriki katika mauaji ya kimbari ya 1994 ambayo yaliua karibu Watutsi milioni moja na Wahutu wenye msimamo wa wastani. M23 inasema inapigana kulinda jamii za Watutsi mashariki mwa Kongo.
Rwanda na DR Congo zilisaini makubaliano ya amani huko Washington mnamo Desemba kama sehemu ya juhudi za Rais wa Marekani Donald Trump za kuleta amani na kuvutia mabilioni ya dola katika uwekezaji wa Magharibi.
Hata hivyo, siku chache baada ya halfa hiyo, waasi wa M23 waliingia katika Mji wa Uvira mashariki mwa Kongo, karibu na mpaka wa Burundi, katika ongezeko kubwa zaidi la vita katika miezi kadhaa.
Baadaye walijiondoa chini ya shinikizo la Marekani. Hata hivyo, Washington ilisema mwezi huu kwamba uwepo wa waasi karibu na mpaka wa Burundi "una hatari ya kuzidisha mzozo huo kuwa vita pana zaidi ya kikanda."

