BANDA MEDIA BLOG

Mamia ya raia waanza kutoroka katika Mji wa Tigray, Ethiopia

 


Katika jiji kuu la Tigray, Mekelle, vijana wengi wamekuwa wakionekana usiku wakiwa na mabegi na mizigo yao kutafuta usafiri wa basi kuelekea Addis Ababa.

Wenyeji wamekuwa wakilalamikia uhaba wa bidhaa muhimu ikiwemo mafuta ambayo yamekuwa yakiuzwaa kwa magendo na kwa bei ya juu.

Waziri mkuu  Abiy Ahmed amenukuliwa akitoa hakikisho kuwa hana nia ya vita ,hata hivyo ,vikosi vya serikaki na Tigray vimekuwa vikijiandaa katika mpaka wa kaskazini mwa Ethiopia, pande zote zikilaumiana kwa uhasama unaoendelea kuonekana.

Amanuel Assefa kamanda wa pili katika uongozi wa wapiganaji wa Tigray, amesema majeshi ya serikali yamekuwa yakizunguka eneo hilo, haya yakijiri miaka minne baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani wa Pretoria uliomaliza vita vilivyodumu kwa karibu miaka miwili huko Tigray.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG