Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema msingi wa chama ni mabalozi, kwani hao ndiyo wanaosimamia wanachama na kuhakikisha kinakuwa imara.
Kenani amesema hayo leo Machi 9,2026 aliposhiriki kikao cha Shina namba tano katika Tawi la Mahaha Kata ya Bunamhala Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mikoa ya chama kukagua uhai wa chama na miradi na kutatua kero za wananchi.
Akizungumza baada ya kusikiliza ajenda ya kikao cha balozi hiyo Kihongosi amesema CCM pekee ndiyo chama chenye mifumo imara ya uongozi kuanzia ngazi ya chini ya shina hadi taifa, akieleza hakuna chana kingine cha siasa chenye mizizi ya aina hiyo.
“Hao ndio msingi wa chama, chama chetu kina mabalozi wengi sana katika mkoa mzima na hao ndio wanaosimamia wanachama na kuhakikisha chama kinakuwa imara.Ndiyo maana tunapofika wakati wa uchaguzi, hatuna wasiwasi wa kushinda,” amesema Kihongosi.
