BANDA MEDIA BLOG

MWANAHABARI ALIYEKUWA AKIZUILIWA TANGU 2024 AACHIWA HURU HUKO BURUNDI

 






Wakili wake amethibitisha hatua hiyo, baada ya Sandra ambaye analiandikia gazeti la La Nova Burundi, kupewa msamaha na kuruhusiwa kwenda nyumbani siku ya Jumatano.

Wakati alipoonekana Mahakamani mwezi Desemba mwaka uliopita katika mji wa Ngozi, alionekana mdhaifu, alikohukumiwa miaka minne jela kwa kupatikana na hatua ya kudharau mamlaka ya nchi na uchochezi.

Alipewa kifungo hicho baada ya mamlaka kumpata na hatia ya kusambaza taarifa kwenye kundi la Whatsapp kuhusu kuwepo kwa ugawaji wa silaha uliotekelezwa na serikali, kwa mujibu wa shirika la Kimataifa linalotetea wanahahari RSF.

Shirika la RSF ambalo limekuwa likishinikiza kuachiwa kwa mwanahabari huyo,  linasema kukamatwa na kufungwa kwake jela ni mwendelezo wa vitendo vya serikali kuwanyanyasa wanahabari nchini Burundi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG