BANDA MEDIA BLOG

MWEMYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI AHUKUMIWA KWA RUSHWA

 


NA MWANDISHI WETU, DODOMA

MAHAKAMA ya Wilaya ya Chemba, mkoani hapa imemtia hatiani Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Babayu, kata ya Babayu Wilaya ya Chemba Bw. Thomas Elia Madumba kwa kosa la kuomba na kupokea hongo kiasi cha Tsh. 260,000/= (Laki mbili na elfu sitini) kutoka kwa Yona Mnjeleza mkazi wa kijiji cha Babayu.

Ilielezwa mahakamani hapo kwamba mshtakiwa huyo kati ya tarehe 17 Januari 2026, na tarehe 20 Januari, 2026 aliomba na kupokea tsh 260,000/= (laki mbili na elfu sitini) ikiwa ni hongo aliyoiomba kutoka kwa Yona Mnjeleza kwa ajili ushawishi wa kumuachia huru babu yake Mzee Mnyangwila Noje ambaye alikuwa amewekwa kizuizini (mahabusu) kwa muda wa siku tatu katika ofisi ya kijiji cha Babayu, Jambo ambalo ni kinyume na Sheria za nchi.

Kesi hiyo ya jinai Na.3546/2026 ya Jamhuri dhidi ya Thomas Elia Madumba iliongozwa na Mheshimiwa Andrew Hayuma Hakimu Mkazi Mfawidhi na kusimamiwa na mawakili wa Serikali Leonard Haule na Dickson Misanjo wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma.

Katika kesi hiyo iliyoamriwa leo Machi 24, 2026 mshtakiwa alishtakiwa kwa kosa moja la Kuomba na kupokea Hongo kinyume na kifungu cha 15(1)(a) (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 rejeo 2023 ikisomwa pamoja na rekebu ya mwaka 2024 GN. 42.

Mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 3 au kulipa faini ya Tsh. 500,000/= (laki tano) na baada ya ombi la wakili wa Serikali kupitia kifungu 15(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura 329 rejeo 2023 ikisomwa pamoja na rekebu ya mwaka 2024 GN. 42, imeamriwa fedha za mtego wa Rushwa zirejeshwe kwa TAKUKURU kiasi cha Tsh 260,000/= (laki mbili na elfu sitini)

Mshtakiwa amelipa faini.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG