BANDA MEDIA BLOG

NGUVU YA MAREKANI KIVITA IPO HAPA, HIZI NI NCHI ZILIZOKWAMA

 


TAARIFA kutoka nchini Iran zinasema mashambulizi mazito katika himaya ya kiongozi wa Iran Khamenei yamesababisha kuuwawa kwa kiongozi huyo.

Marekani ina historia ndefu na tata ya kijeshi tangu kuanzishwa kwake. Nguvu yake ya kijeshi imetokana na mchanganyiko wa teknolojia ya kisasa, bajeti kubwa, na ushawishi wa kijiografia.
Vita vya Marekani na Uhispania 1898 viliifanya Marekani kuanza kutawala maeneo ya nje kama Philippines na Puerto Rico. Baadaye ilishiriki Vita Kuu vya Kwanza na vya Pili vya Dunia, ambapo iliibuka kama "nguvu kuu" (superpower).
Vita Baridi na Mapambano dhidi ya Ukomunisti, kulikuwa na uvamizi na mivutano kama Vita vya Korea (1950s) na Vita vya Vietnam (1960s/70s).
Marekani inatajwa kuwa na jeshi lenye nguvu zaidi duniani kutokana na vigezo vifuatavyo.
Bajeti ya Kijeshi, Mfano Marekani ilitumia zaidi ya $800 bilioni kwa mwaka (2024/2025), kiasi ambacho ni kikubwa kuliko nchi 10 zinazofuata zikijumlishwa.
Teknolojia, Inaongoza kwa ndege za kivita zisizoonekana kwenye rada (Stealth Technology), mifumo ya kisasa ya makombora, na matumizi ya AI vitani.
Nguvu ya Majini, Marekani Ina Manowari za Kubeba Ndege (Aircraft Carriers) 11, zinazoifanya iweze kushambulia popote duniani ndani ya muda mfupi.
Vituo vya Kijeshi, Marekani pia Ina zaidi ya vituo 750 vya kijeshi katika nchi zaidi ya 80 duniani, jambo linaloipa uwezo wa kudhibiti maeneo mbalimbali kwa urahisi na kwa muda mfupi.
Silaha za Nyuklia, Ina akiba kubwa ya silaha za nyuklia (takriban 5,000+), inayofanya nchi nyingine kuogopa kuivamia moja kwa moja.
Ukitaka kujua Marekani wananguvu kiasi gani za kijeshi ziulize hizi nchi 😃😃
Marekani iliwahi kuivamia Mexico na kushinda mfululizo wa mapambano hadi kuuteka mji mkuu Mexico City. Ushindi huu uliilazimisha Mexico kusaini mkataba wa kuipatia Marekani zaidi ya 50% ya ardhi yake na Marekani walifanikiwa kuyapata maeneo ambayo kwa sasa ni sehemu ya Marekani California, Nevada, Utah, Arizona, na New Mexico.
Marekani waliwahi kuzichapa na Hispania
Hii ilikuwa vita fupi sana (miezi mitatu na wiki tatu). Marekani ililishinda vibaya jeshi la majini la Uhispania. Matokeo yake, Uhispania ilipoteza himaya yake ya mwisho huko Amerika na Pasifiki, na Marekani ikachukua udhibiti wa Puerto Rico, Guam, na Philippines, huku Cuba ikipata uhuru wa jina chini ya usimamizi wa Marekani.
Ujerumani na Japan (Vita Kuu vya Pili vya Dunia, 1941–1945)
Huenda huu ndio ushindi mkubwa zaidi wa kijeshi wa Marekani katika historia. Marekani, ikishirikiana na washirika wake (Uingereza na Urusi), iliivamia Ulaya na kuilazimisha Ujerumani ya Nazi kusalimu amri bila masharti.
Japan: 1945 Baada ya mapambano makali ya majini na ardhini, Marekani ilitupa mabomu ya nyuklia huko Hiroshima na Nagasaki, jambo lililoipelekea Japan kusalimu amri mara moja.
Iraq (Vita vya Ghuba - Gulf War, 1990–1991)
Wakati Saddam Hussein alipoivamia Kuwait, Marekani iliongoza muungano wa nchi 35. Katika operesheni iliyoitwa Desert Storm, Marekani ililishinda jeshi la Iraq ndani ya saa 100 tu za mapambano ya ardhini na kuikomboa Kuwait. Huu unatajwa kama moja ya ushindi wa kijeshi wa haraka na wa kiteknolojia zaidi.
Marekani wameichachafya Iran ndani ya muda mfupi, kila kitu kimebadilika.

chanzo nyanza news

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG