BANDA MEDIA BLOG

Vita vya Mashariki ya Kati: Mazishi ya kitaifa ya Ayatollah Khamenei yaahirishwa Iran

 


Iran imeamua Jumatano, Machi 4, kuahirisha mazishi ya kitaifa ya Kiongozi Mkuu wa kiroho Ali Khamenei, yaliyopangwa kufanyika jioni huko Tehran, huku nchi hiyo ikikabiliwa na mashambulizi makubwa ya anga ya Israel na Marekani.

"Sherehe ya kumuaga imamu aliyeuawa shahidi imeahirishwa (...) kwa kutarajia idadi isiyo ya kawaida ya watu kujitokeza," televisheni ya serikali imesema, ikiongeza kuwa tarehe nyingine "itatangazwa baadaye."

Mapema leo Jumatano asubuhi, swala ya mwili (Salat al-Janazah) ya Ali Khamenei ilitangazwa jioni ya leo huko Tehran. Alifariki akiwa na umri wa miaka 86 katika shambulio la Israel na Marekani na atazikwa katika mji mtakatifu wa Mashhad, kaskazini mashariki mwa nchi, mahali alipozaliwa.

Wakati huo huo, Israel imetangaza leo Jumatano kwamba imezindua "wimbi kubwa" la mashambulizi mapya dhidi ya Iran, huku vita katika Mashariki ya Kati vikiingia siku yake ya tano. 

Lebanon pia iliathiriwa. Milipuko mingi imesikika nchini humo, ambayo tayari ilikuwa imerekodi vifo kumi asubuhi na mapema. 

Iran inaendelea kurusha makombora dhidi ya Israel na nchi za Ghuba kama kulipiza kisasi. Athari inayoongezeka ya mzozo wa kikanda inasababisha bei ya mafuta kupanda na kutisha masoko, haswa barani Asia, ambapo soko la hisa la Seoul limesitiishwa baada ya kushuka kwa kasi.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG