BANDA MEDIA BLOG

WANAWAKE MANYARA WANUFAIKA KWA MIKOPO

 


                                          Na Mwandishi wetu, Simanjiro

WANAWAKE wa Mkoa wa Manyara, wamenufaika kiuchumi kupitia fedha za mikopo kwa kupokea Sh4.2 bilioni kwa muda wa miaka mwili ya miaka ya fedha ya 2024/2025 na 2025/2026.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga ameeleza hayo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa yamefanyika kwenye kijiji cha Orkirung’rung’ Kata ya Edonyongijape Wilayani Simanjiro.

 RC Sendiga ameeleza kuwa wanawake hao wamenufaika kupitia mikopo hiyo ya Sh3 bilioni zilizotolewa mwaka 2024/25 na mwaka 2025/26 hadi mwezi Februari zimeshatolewa Sh1.2 bilioni.

“Hongereni sana wanawake wa Manyara mnajituma na kupitia kauli mbiu ya Haki na usawa kwa wanawake na wasichana msingi jumuishi kufikia dira 2050,” amesema.

 Hata hivyo, amewaasa wanawake kutumia mbinu 223 na siyo mbinu moja za kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika familia zao

“Mwanamke anapaswa kuleta mabadiliko ya dunia kila mahali alipo na usisubiri uwe kiongozi na dunia itakuwa njema zaidi kupitia mwanamke,” amesema RC Sendiga.

Amesema wanawake wanapaswa kung’ara katika nyanza zote ikiwemo kiuchumi, kiuongozi, kielimu, kimalezi ya watoto, kuondokana na watoto wenye utapiamlo na wenye udumavu.

“Wakina baba hawali chakula na kushiba nyumbani, mnawaacha wazunguke na vichupa vya pombe mitaani, bado wanawake wanapaswa kuwatunza wanaume,” amesema RC Sendiga.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Fakii Lulandala amekabidhi tuzo kwa mkuu huyo mkoa ya kutambua uongozi thabiti na utawala bora.

“Wanawake wa mkoa wa Manyara wametambua juhudi zako katika kujitoa kwako na kuhakikisha jamii unayoingoza inapata maendeleo na kuishi kwa amani na utulivu,” amesema.

Msoma risala Belinda Sumari amesema pamoja na jitihada za serikali kuwajengea uwezo wa kiuchumi kwa wanawake wamepatiwa elimu ya malezi na makuzi, haki za wanawake na kupinga ukatili.

Hata hivyo, amesema bado wanawake na wasichana wana changamoto za ukosefu wa mitaji ya kuanzisha ujasiriamali katika eneo hilo.

Amesema wanawake wa mkoa wa Manyara wanaendelea kupambana na ndoto zao na ndogo za watoto wao zisizimwe na changamoto kwani kila changamoto ni daraja la kufikia mafanikio makub

“Bado changamoto za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo ukeketaji na ushiriki mdogo wa wanawake katika nafasi za uongozi inayosababisha kushindwa kushiriki katika ngazi za maamuzi,” amesema.

Baadhi ya wadau wa maendeleo wa mkoa huo Taiko Kulunju na Mula Sanare Lesiangiki wamepatiwa vyeti vya kufanikisha maadhimisho hayo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG