.................
Machi 9, 2026 wanawake katika Ofisi Kuu ya Dayosisi ya Central Tanganyika Dodoma - Mackay House wameungana na wanawake wengine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8, ya kila mwaka.
Katibu wa Ushirika wa wanawake wa Kikristo DCT UWAKI Rev. Happiness Mkangala amesema, wamelazimika kufanya sherehe hizo zilizoambatana na Ibada maalum leo machi 9 kwa lengo la kuungana na kaka zao.
Akihubiri katika ibada hiyo Kasisi Anna Yohana wa Parishi ya Ntyuka Mlimani amemuelezea mwanamke kuwa ni mama katika familia anayevaa nyazifa za mwalimu, Daktari na shujaa. Ni shujaa kwasababu ya wingi wa majukumu aliyonayo.
Mathayo anaandika juu ya wito wa mwanamke, akasema wanawake wanatakiwa kupata pumziko katika YESU Kristo, shughuli alizonazo mwanamke ni nyingi sana, anatakiwa awe mama hata kama akiwa na huzuni kiasi gani, "mama amepitia magumu ambayo hatakiwi kutabasamu yeye atatabasamu", anasema
Amesema mama ana wajibu mkubwa zaidi kuliko wanavyofikiri, anawazia watoto hata kama hawako nae, wanawake Wengi wako Katika mashaka na mahangaiko mengi, lakini wakiwa ndani ya Kristo hawatakuwa na mashaka, YESU atawapumzisha,
Kasisi Anna akawaalika wanawake wote wamtafte YESU kwa bidiii, badala ya kusumbuka na mambo mengi ya Dunia hii kama tamaa za kutaka mambo makubwa yanayopelekea kuingia katika vikundi vya vikoba matokeo yake wanakimbizwa na mikopo n.k
Kasisi Anna akahitimisha kwa kusema kama wakikubali kumfuata YESU, basi, Yesu Kristo yuko tayari kuwatia nguvu.
Aidha, Mhashamu Askofu Dkt Chilongani aliwataka wanawake kuwa waangarifu kusimamia maadili ya kwao wenyewe na watoto wao japo wengi wanasahau wanaume zao, badala yake waaangalia watoto wao zaidi.
Akawataka waanze kuangalia wanaume zao ndipo wafuate watoto.
Wanawake ni Jeshi kubwa











