*STAMICO KINARA KUENZI MAONO YA MWALIMU J. K NYERERE KATIKA KONGAMANO LA VIJANA NA MWALIMU J. K NYERERE DODOMA*.
Leo tarehe 11 Aprili, 2026 Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa tuzo kwa Shirika la Madini la Taifa kwa kuthamini mchango wa Shirika katika kuenzi maono ya Mwalimu J.K Nyerere . Sambamba na hilo Makamu wa Rais amewaasa Vijana kuwa waadilifu ,kutunza Amani na kupiga vita rushwa kwa kuwa ni adui wa Taifa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse akichangia maada katika Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere lililoandaliwa na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu J.K Nyerere amewaasa Vijana na washiriki kuyaishi na kuenzi Maono ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius K. Nyerere .
Dkt.Mwasee alifafanua Shirika limeanzishwa tarehe 12 Agosti, 1972 na hati yake imesainiwa na Mwalimu Nyerere. Katika kipindi kifupi cha mabadiliko ya kiutendaji Shirika limeweza kuajili zaidi ya wafanyakazi 1000 na wengi wao ni Vijana.
Akaendelea kusema, zaidi ya nchi 5 zimekuja STAMICO ilikujifunza namna ya kuanzisha na kuendesha mashirika ya Umma ya madini . Hata hivyo katika kipindi kifupi nchi Tatu (3) kati ya hizo zimeshafanikiwa kuanzisha mashirika tayari. Hii inaonesha namna maono ya Mwalimu Nyerere yanaishi na mfano wa kuigwa barani Afrika.
Katika kuhakikisha STAMICO inatekeleza Dira ya Taifa ya 2050 .Shirika limewezesha taasisi mbali mbali za Vijana kupitia vifaa na maarifa ilikunufaika na sekta ya madini kwa ajili ya kuchangia Dira ya Taifa ili kufikia lengo la serikali la kitaifa la kipato cha Dola za Kimarekani (USD) trilion moja na kipato cha kila mtanzania kuwa USD 7000 kwa mwaka.
Aidha Mhe. Waziri Mkuu Mstaafu Mizengwe P. Pinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere amewasihi Vijana kusoma historia ya Taifa la Tanzania. Itawasaidia kujua mchango waliochangia maendeleo ya Taifa na kuwaenzi.Pia amewaamasisha kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa.
Kongamano la Vijana na Mwalimu Nyerere lililofanyika Jiji Dodoma katika ukumbi wa Chimwaga, UDOM liliambatana na shughuli za upandaji miti ambapo Viongozi mbali mbali walishiriki .