BANDA MEDIA BLOG

WAKRISTO WAASWA KUENDELEA KUTENDA MATENDO MEMA



 Askofu Mkuu wa Makanisa ya C.E.C.T na Mwenyekiti mweza Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoani Mwanza Charles Sekelwa.


………

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wakristo Mkoani Mwanza wameaswa kuendelea kutenda matendo mema kwenye jamii hata baada ya Pasaka hatua itakayosaidia kuwa na hofu ya Mungu moyoni mwao.
Rai hiyo imetolewa leo Alhamisi Aprili 02, 2026 na Askofu Mkuu wa Makanisa ya C.E.C.T na Mwenyekiti mwenza Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoani Mwanza, Charles Sekelwa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelekea katika sherehe za Pasaka.
Amesema matendo mema wanayoyatenda wakristo wakati wa kipindi cha Kwaresima yanapaswa yaendelee kufanywa hata baada ya sherehe za Pasaka.
“Katika kipindi cha Kwaresima tunatubu na tunakuwa tunaomba rehema kwa Mungu atukaribishe tuwe karibu nae  ili maombi yetu ayasikie na kutuondoa katika changamoto mbalimbali tunazopitia”, Amesema Askofu Sekelwa.
Amesema wakifanya matendo mema wakati wa kipindi cha Kwaresima tuu na baada ya pasaka wakarudia kufanya matendo yasiyompendeza Mungu watakuwa wameikana Imani.
Ameeleza kuwa matendo mema ni pamoja na kuwasaidia wahitaji,yatima na kuwatia moyo watu waliokata tamaa.
Aidha, amewaomba kusherehekea  sikuku ya Pasaka kwa njia iliyobora na kwaheshima ili kuepuka changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG