BANDA MEDIA BLOG

WANANCHI KATA YA KILIMANI WABAINISHA CHANGAMOTO HIZI KWENYE MKUTANO WA DIWANI

Na Barnabas Kisengi Dodoma 

 UBOVU wa Miundombinu ya Barabara, Uchakavu wa mabomba ya maji yanayovujisha maji kutokana na kutoboka pamoja na Taka kutozolewa na kampuni ya usombaji taka vimeibuka kwenye ziara ya Diwani wa kata ya Kilimani, jijini Dodoma Mussa Mkunda wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi wa kata hiyo.

Kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Aprili 18,2026 katika mtaa wa Image wakazi wa mtaa huo wameilalamikia mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira (Duwasa) kwa kushindwa kuziba bomba kubwa la maji lililopasuka kwa muda mrefu sasa ambapo maji yamekuwa yakitiririka na kusababisha hasara kati yao na Mamlaka hiyo, wakati Tarula hawajashulikia kero ya ubovu wa barabara pamoja na kutowawekea Taa za barabarani hali ambayo wanaona ni hatari kwa nyakati za usiku.

 "Hili swala la bomba kupasuka limekuwa kero kubwa kwetu licha ya kutoa taarifa kwenye mamlaka husika pamoja na wataalamu wa Duwasa kufika lakini hatujaona hatua zozote zilizo chukuliwa hadi Sasa jambo ambalo tunalihofia kuwa bomba hili likizidi kupasuka litaleta athari kubwa katika makazi,

miundombinu ya barabara za mtaa wetu sio rafiki jambo ambalo wakazi wenye vyombo vya moto wanashindwa kuingia katika baadhi ya maeneo yetu kwenye mtaa hata tunapo kuwa na mgonjwa huwa ni shida kuingia katika maeneo yetu amesema moja wa wananchi hao,

Mhe Diwani na wataalamu wako tena tumeona viongozi wa chama hapo mtusaidie kutatua changamoto hizi kwetu imekuwa kero ya muda mrefu licha ya kuripoti kwa viongozi wetu wa mtaa sasa tunaamini kuwa viongozi wa CCM kata na wataalamu kutoka kata sasa tunaamini kuwa tutapata ufumbuzi wa changamoto zetu Ipasavyo”,Mzee Sebastian Chambasi

Changamoto ya takataka zilizozagaa katika maeneo ya mitaa hiyo zikatajwa kuwa ni hatari kwa afya na kwamba zinaweza kusababisha maganjwa ya mlipuko, ikiwemo hatari ya kuvamiwa na kuraruliwa na mamba wanaoonekana kwenye mtaro mtaani humo.

Diwani wa kata hiyo Mussa Mkunda akawatoa hofu kwa kuzichukua chanagamoto hizo na kuahidi kwenda kwenda kuzifanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kumwelekeza afisa mifugo wa kata hiyo Tabia Shani kuwasiliana haraka na watu wa maliasi ili kuweza kutatua changamoto hiyo ya Mamba kwa haraka ili isije ikasababisha maafa katika mtaa huo kutokana na wananchi wanao vuka katika korongo hilo.

"Ndugu zangu wananchi wa mtaa wa image niwapongeze sana kwa kuweza kuelezea changamoto za mtaa wenu niwahakikishie Mimi kama Diwani wenu hapa zimefika na tunakwenda kuzifanyia kazi kwa haraka nitahakikisha Mimi na wataalamu wangu tulio ongozana nao pamoja na viongozi wa Chama cha mapinduzi ambacho ndicho tunatekeleza ilani yake”, amesema

Kwa upande Wake katibu wa chama cha mapinduzi CCM kata ya kilimani  Ramadhani Ramadhani amesema kuwa kama chama ndicho chenye ilani inayotekelezwa kwa kipindi Cha 2025/2030 wao kwa kushirikiana na serikali watahakikisha changamoto zote zilizojitokeza kwenye mkutano huo zinafanyiwa kazi kwa haraka ili kuweza kuhakikisha wananchi wanakuwa katika mazingira mazuri na salama kwenye Mtaa huo.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG