BANDA MEDIA BLOG

Watu 43 wameuawa katika shambulio la ADF kaskazini mashariki mwa Congo


 Na:


Mauaji haya yamethibitishwa na msemaji wa jeshi la serikali FARDC katika mkoa wa Ituri Luteni Jules Tshikudi Ngongo.

Luteni Ngongo amesema mbali na watu hao kuaawa, nyumba 44 zimeteketezwa moto katika shambulizi lilitokea wiki hii katika êneo la Bafwakoa, wilayani Mambasa.

Waliouwa walikatwa kwa mapanga huku wengine wakiteketezwa kwa moto wakiwa ndani ya nyumba zao na wengine kutekwa na waasi hao wa ADF.

Mkuu wa Wilaya ya Mambasa, Baptiste Munyapandi, amesema operesheni inaendelea kuwatafuta watu ambao hawaonekani mpaka sasa, na huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Mashambulizi ya ADF yameendelea kushika kasi katika miezi ya hivi karibuni jimboni Ituri na Kivu Kaskazini, licha ya eneo hilo kuwepo kwa kikosi cha pamoja cha wanajeshi wa Uganda na DRC tangu mwaka 2021 wanaoendeleza operesheni shujaa, kuwakabili waasi hao wenye asili ya Uganda.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG