BANDA MEDIA BLOG

WATU WENYE ULEMAVU JIMBO LA MTUMBA KUWEZESHWA MIRADI YA KIUCHUMI

 

                           NA MWANDISHI, WETU MTUMBA DODOMA

                                            .........................

MBUNGE wa jimbo la Mtumba jijini Dodoma Athoni Mavunde amesema Watu wenye ulemavu wa Jimbo la Mtumba jijini Dodoma kupitia programu za uwezeshwaji kiuchumi watapatiwa mikopo ya serikali kuwezeshwa miradi ya kiuchumi ili waweze kujitegemea na kujiendeleza kiuchumi.


Ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya usaidizi kwa watu wenye ulemavu wa Jimbo la Mtumba.

Tunamshukuru Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuwajali na kuwaendeleza watu wenye ulemavu nchini.

Suala la mikopo na uwezeshwaji kiuchumi watu wenye ulemavu ni ukombozi mkubwa katika kuwafanya waweze kujitegemea.

Jimbo la Mtumba tumeandaa programu mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kiuchumi.

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye Ulemavu(SHIVYAWATA) Mkoa wa Dodoma Ndg. Omar Lubuva ameishukuru serikali kwa namna ambavyo imekuwa mstari wa mbele kutatua changamoto za watu wenye ulemavu,pia amemshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada wa viti mwendo na fimbo nyeupe kwa watu wenye ulemavu kwa kuwa hiyo ni hatua kubwa katika kupunguza changamoto za watu wenye ulemavu.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma,Ndg. Sakina Mbugi amesema serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na watu wenye ulemavu katika utatuzi wa changamoto zao pamoja na kuendelea kuongeza fursa za kiuchumi kwa kundi hili.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG