NA JOHN ISRAEL
Chama cha Afya ya
Akili Afrika (AMHA) Kimeutangaza mwezi Mei 2026 kuwa mwezi wa maadhimsho ya Uhamasishaji
wa Afya ya Akili, huku msisitizo ukiwa kwenye kupunguza unyanyapaa, na kukuza
mikakati ya kuboresha hali ya Akili kwa vitendo katika nchi zote za Afrika
na kwingineko Duniani.
Katika taarifa iliyotufikia
katika meza yetu ya habari imebainisha kuwa Kauli mbiu ya mwaka huu, ni kila mtu Kutumia
Rasilimali Zake Binafsi Kukuza Afya ya Akili yake, ikisisitizwa kuwa uwezo ambao
kila mtu anao katika kudumisha na kuboresha hali yake ya kiakili.
Taarifa hiyo
imeonyesha kuwa Katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi na wenye shinikizo la
kiuchumi, changamoto za kijamii, na kuongezeka kwa wasiwasi wa afya ya akili,
ni muhimu kwa watu binafsi na jamii kutambua na kutumia uwezo wao wa ndani na
mifumo ya usaidizi inayopatikana.
Pamoja na kuwa Afya
ya akili ni muhimu, emeelezwa kuwa inapuuzwa katika nchi nyingi za Kiafrika,
ambapo Hali kama vile mfadhaiko, wasiwasi, matatizo ya matumizi ya vileo, na
magonjwa yanayohusiana na mfadhaiko yanaendelea kuathiri mamilioni ya watu,
hata hivyo upatikanaji wa huduma, ufahamu na kukubalika bado ni mdogo.
AMHA inaamini kuwa
kuwawezesha watu binafsi kwenye maarifa, ujuzi, na usaidizi kunaweza
kubadilisha matokeo kwa kiasi kikubwa na kujenga jumuiya thabiti.
Katika mwezi mzima wa Mei, AMHA itaongoza na kuunga mkono mfululizo wa shughuli zinazolenga kutoa elimu, utetezi, na ushiriki kwa jamii, kwa mtililiko huu, wa Programu za uhamasishaji kwa jamii, Kampeni za elimu ya afya ya akili shuleni, mahali pa kazi, na kwenye mashirika ya kidini.
Adha kuendesha Mijadala kwenye vyombo vya habari pamoja na umma kwa ujumala wake, kufanya Vikao vya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa afya na watu wa kujitolea kwenye jamii, kufanya Kampeni za kidijitali za kukuza tabia za kujitunza na kutafuta usaidizi.
Kama sehemu ya kampeni hii, AMHA inawahimiza watu binafsi kuchukua hatua rahisi lakini zenye matokeo ili kusaidia afya yao ya akili kwa kukuza uelewa na kujitambua kunakoleta mabadiliko ya kihisia, pia kudhibiti Mfadhaiko, pamoja na kujizoesha kukabiliana na hali za kiafya kama vile mbinu za kustarehesha pamoja na kudhibiti wakati.
ikiwa ni pamoja na kujenga Mahusiano Chanya, Kukuza miunganisho ya kijamii yanayounga mkono yenye maana, kuendelea Kujishughulisha, kushiriki katika shughuli za kimwili zinazokuza ustawi wa kimwili na kiakili, kutafuta Usaidizi Unapohitajika, Wasiliana na wataalamu, watu binafsi wanaoaminika au huduma za usaidizi bila kusita.
AMHA inatoa wito kwa serikali, watunga sera, taasisi za huduma za afya, mashirika ya kiraia, na washirika wa maendeleo kutanguliza afya ya akili kwa kuwekeza katika huduma zinazofikiwa, nafuu na zinazofaa kitamaduni za afya ya akili. Kuimarisha mifumo ya afya ya akili sio tu kipaumbele cha afya lakini pia ni hitaji la kijamii na kiuchumi.
Pia imehimiza vyombo
vya habari vichukue jukumu la kuwajibika katika kuunda uelewa wa umma wa afya
ya akili kwa kutangaza habari sahihi na kupunguza unyanyapaa. Afya ya akili ni
jukumu la kila mtu. Kwa kuchukua hatua ndogo, za makusudi na kusaidiana,
tunaweza kujenga watu binafsi, familia na jumuiya imara.
Kwa pamoja, hebu
tuunde siku zijazo ambapo afya ya akili inathaminiwa, inalindwa, na kukuzwa kwa
wote.

